November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Watahiniwa 393 wafutiwa matokeo mtihani darasa la saba

Spread the love

 

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA), limefuta matokeo ya watahiniwa 393, waliobainika kufanya udanganyifu wakati wa kufanyika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumamosi, tarehe 30 Oktoba 2021 na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde, akitangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba, uliofanyika tarehe 8 na 9 Septemba mwaka huu.

“NECTA limeyafuta matokeo ya watahiniwa 393, waliobainika kufanya udanganyifu wakati wa kufanyika mitihani hii ya kumaliza elimu ya msingi, kwa mujibu wa kifungu cha 30 (2B ) cha kanuni za mitihani,” amesema Dk. Msonde.

Aidha, Dk. Msonde amesema NECTA limezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 128, ambao walishindwa kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo kuugua au kupata matatizo. Hivyo, wamepewa fursa ya kurudia kufanya mtihani 2022.

error: Content is protected !!