October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watafiti wa Kilimo: Tukizuiwa kufanya kazi, tujiandae na njaa, umaskini

mazao la Alizeti

Spread the love

WATAALAMU wa tafiti za mbegu bora za kilimo Tanzania, wametaadhalisha kuwa kuenea kwa kasi kwa virusi hatari vya ugonjwa wa Corona huenda ukaathiri tafiti za kilimo Tanzania, hali ambayo itapelekea njaa na umaskini hapa nchini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Wamesema kwamba, endapo wakulima watazuiliwa kushiriki katika tafiti mbalimbali zinazoendelea kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona, kuna uwezekano mkubwa wa kuathiri shughuli za utafiti ikiwemo upatikana wa mazao bora mashambani.

Mtafiti na Mzalishaji Mkuu wa mbegu katika kituo cha tafiti za kilimo Tanzania (TARI), kituo cha Hombolo, Dk. Lameck Nyaligwa, amesema kuna haja kubwa ya Serikali kuwaruhusu wataalamu wa tafiti za mbegu bora za mazao kuendele na shughuli zao za kitafiti ambazo kimsingi zinahitaji mjumuiko mkubwa wa wakulima husika.

Dk. Nyaligwa ametoa wito huo kutokana na katazo la serikali la mkusanyiko wa watu wengi katika maeneo mbalimbali na hasa mkusanyiko usiokuwa wa lazima ikiwa ni juhudi za kupunguza kasi ya maambizi ya ugonjwa wa Corona Duniana, na Tanzania kwa ujumla.

“Tafiti za mbegu kwa kiasi kikubwa zinahitaji ushirika wa wakulima husika, wakati mwigine zaidi ya wakulima 100, hivyo tunaiomba Serikali kufikiria jambo hili,” alisema.

Pamoja na ombi hilo, aliongeza kuwa ni kweli kwamba sekta ya kilimo imeajiri takribani asilimia 80 ya Watanzania, na inachangia asilkimia 30 ya pato la taifa ni muhimu kwa watafiti sekta hiyo muhimu waendelee na tafiti zao.

“Kwa mfano, TARI-Hombolo tangu mwaka jana imeanza kutekeleza tafaiti mbalimbali za mbegu bora za mazao ya mtama, alizeti  na uwele kwa ushikiano na mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, miradi ya gharama kubwa na yenye umuhimu mkubwa katika kuendelezaji sekta ya kilimo nchini,” aliongeza.

Aidha alisema, miradi hiyo ambayo kwa sasa inatekelezwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini, inahitaji wataalamu  husika kusafiri na kukutana na wakulima ili kuwezesha mbegu hizo zilizo katika majaribio kuthibitidshwa na mamlaka ya taifa ya kuthibisha ubora wa mbegu (Tosci).

error: Content is protected !!