Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wataam watakiwa kumaliza makosa ya mitandaoni
Habari Mchanganyiko

Wataam watakiwa kumaliza makosa ya mitandaoni

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Andikie
Spread the love

WIZARA ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, imewaomba wataalamu wa masomo ya kompyuta kuzingatia mafunzo wanayofundishwa ya mafunzo ya makosa ya mtandao, itasaidia kuondoa migogoro ya watumiaji, anaandika Angel Willium.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, katika uzinduzi wa semina ya mafunzo ya makosa ya mtandao Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Andikie, amesema wanatakiwa kuzingatia mafunzo wanayopewa na kufanya kwa vitendo lengo nikutokomeza mashambulizi yanayoendelea mitandaoni.

“Mkutano huu umelenga kuwapa mafunzo wataalamu wa mtandao na kubadilishana uzoefu na mataifa ya Uarabuni, Asia na Afrika,” amesema Andikie.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCAR) James Kilaba amesema wanayo madarasa kwa ajili ya wataalamu wajifunze kwa kirefu na wanaendelea kujifunza kwa sababu mara nyingi mambo ya mtandao hubadilika.

Pia Kilaba amesema wanashirikiana na mataifa mbalimbali ili kuweza kuzuia makosa ya mtandao, hivyo tatizo likitokea siyo lazima liletwe kwenye ofisi zao, hata nchi nyingine inaweza kutatua na wana vifaa vya kutosha ambavyo vinaboreshwa kutokana na kubadilika kwa matumizi ya mtandao.

Semina ya mafunzo ya makosa ya mtandao yanafanyika kila mwaka, yalianza 2014 wataalamu wa mtandaoni upewa mafunzo na kisha wanajifunza wenyewe kwa vitendo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!