Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wataafu TRL walilia mafao yao
Habari Mchanganyiko

Wataafu TRL walilia mafao yao

Spread the love

WAFANYAKAZI wastaafu zaidi ya 100 wa kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kuanzia mwaka 2012 hadi  2017 wamemuomba Rais John Magufuli kuingilia kati kitendo cha kunyimwa stahiki zao kwa wakati ikiwemo mafao yao ya kustaafu, anaandika Christina Haule.

Wakizungumza kwa niaba ya wenzao, Wastaafu hao wa kampuni ya reli mkoani Morogoro wamesema kuwa wanaidai kampuni hiyo fedha za mizigo na nauli ya kuwarudisha makwao, tuzo ya utumishi wa muda mrefu, tuzo ya kustaafu na mifuko ya hifadhi za jamii ya PPF na NSSF.

Hata hivyo jana katika kikao cha wastaafu wa reli mkoani hapa, Mwenyekiti wa Wafanyakazi wastaafu wa kampuni ya reli, Emily Msafiri alisema kuwa tatizo hilo limezidi kuwa kubwa tangu shirika hilo lilipobinafsishwa na hivyo kusababisha usimamizi kuwa mdogo.

“Sasa hivi ukistaafu unakaa muda mrefu ndio ulipwe,hali imebadilika toka shirika libinafsishwe, usimamizi umekuwa mdogo, tulipokuwa bado tupo kazini tulikuwa hoi kwa kazi nyingi, lakini leo hawatuthamini” alisema Msafiri.

Kwa upande wake Katibu wa wafanyakazi wastaafu wa Kampuni ya reli Morogoro, Selungwi Ubwe alisema kuwa wanaishi maisha magumu sana huku wengi wao wakiwa wadhaifu na wengine tayari wameshafariki dunia kwa kukosa fedha za kujikimu na kuacha wajane na watoto wakiteseka bila kupata msaada wowote.

Ubwe alisema kuwa wanamuomba Rais John Magufuli kuingilia kati na kuwasaidia kupata stahiki zao kwani Mwajiri wao anasema Shirika halina fedha za kuwalipa hata tuzo zao za kustaafu huku akidai ni haki yao.

Ubwe alisema anachoshangazwa na TRL kwa sasa ni suala la kuambiwa kampuni haina hela mpaka wasubiri wauze vyuma chakavu ndio walipe deni hilo la tuzo ya kustaafu ndani ya miezi ya sita.

“ Kikubwa zaidi ni hiyo tuzo ya kustaafu ambayo mfanyakazi anapostaafu anatakiwa kulipwa mshahara mmoja kwa mwaka mara utumishi wake, hilo limekuwa ndoto, tangu 2012 ni wachache ndio wamelipwa tena mahakamani” alisema Ubwe.

Nao Wajane ambao waume zao ni wastaafu wa reli Yustina Nanyansi na Aive Timoleta wamedai kupata shida na watoto na wanapofatilia mafao ya waume zao wanazungushwa bila kupata chochote huku siku nyingine wakiambiwa wameshalipwa au shirika halina fedha.

Mjane mmoja Yustina alisema huku akilia kwa uchungu kuwa hata nyumba ambayo marehemu mume wake aliinunua kutoka shirika la reli kwa sasa anaambiwa bila kupata risiti hatatambulika kama mmiliki wa nyumba hiyo.

Hata hivyo Ofisa mawasiliano wa kampuni ya reli Tanzania Mohamed Mapondela alipotafutwa kuelezea sakata hilo aligoma kuongea na waandishi wa habari akidai kupewa kwanza majina ya wastaafu wote wanaolalamikia madai hayo ndipo yeye atakapoweza kujua ajibu nini, huku akisema kuwa kama ni madai ofisi zote zina madai.

“Ni kweli kuna watu hatujawalipa, nipe majina nimrushie afisa mwajiri tujue wangapi wameshalipwa, nitajibu nini sasa, ungekuwa wewe ungejibu nini kwa mfano” alijibu Mapondela.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!