May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wastaafu  wapigwa hela za mafao 400 Mil., Serikali yaingilia kati

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamadi Masauni

Spread the love

 

MBUNGE wa Jang’ombe visiwani Zanzibar, Ali Hassan King, amefikisha bungeni kilio cha wastaafu 103, walioibiwa fedha zao za mafao Sh. 400 milioni na baadhi ya watumishi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akizungumza katika kipindi cha maswali na majibu, bungeni jijini Dodoma, leo Ijumaa tarehe 9 Aprili 2021, King amedai kuwa, fedha hizo ziliibiwa na baadhi ya watumishi wa NBC katika Tawi la Forodhani visiwani Zanzibar.

Na kuhoji lini Serikali italishughulikia suala hilo ili wastaafu hao walipwe fedha zao.

“Lini Serikali itawalipa wateja 103 ambao fedha zao kiasi cha Sh. 400 mil. ziliibwa na watumishi wa NBC wa Forodhani, lakini pamoja na kuichukulia hatua au kuipa adhabu hiyo benki kwa kutolipa wateja hawa?” amehoji King na kuongeza:

“Ili kuhakikisha hawa wazee wanalipwa fedha zao za kiinua mgongo ambao wengine wameshafariki, je Serikali iko tayari kufuatilia kwa haraka pamoja na mimi, kuhakikisha kwamba haya wanayosema yanatokea?”

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhandisi Hamad Masauni, ameahidi kulishughulikia suala hilo kwa kushirikiana na mbunge huyo, ili kujua hatua gani zimefikiwa katika kufikia utatuzi wake.

“Kwa sababu suala hili si mahsusi,  ninahitaji kufahamu kwa undani hasa kujua wizi huu chanzo chake ni nini na uchunguzi huu kama umefanyika umefika hatua gani.  Ili tutoe maelekezo hatua ziweze kuchukuliwa,” ameahidi Mhandisi Masauni.

Kuhusu benki hiyo kuchukuliwa hatua kwa kushindwa kuwalipa wastaafu hao,  Mhandisi Masauni amesema Benki Kuu ya Tanzania ( BoT).

“Kama suala hili limesababishwa na watumishi wa benki hatua zitachukuliwa, kama limesababishwa na mifumo ya benki, BoT itachukua dhamana ya kuhakikisha zinarudishwa na itaichukulia hatua benki husika,” amesema Mhandisi Masauni.

error: Content is protected !!