Wednesday , 21 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Wastaafu waililia Serikali ya JPM
Habari Mchanganyiko

Wastaafu waililia Serikali ya JPM

Spread the love

ZAIDI ya wastaafu 300 kutoka wilaya za Nyamagana na Ilemela Mkoani Mwanza, wameilalamikia Serikali kwa kuwakata makato makubwa ya pensheni zao za kila miezi mitatu kwani hayaendani na hali halisi ya maisha, anaandika Moses Mseti.

Wakizungumza leo katika zoezi la kufanyiwa uhakiki, linalofanywa na Wizara ya Fedha na Mipango wamedai kwamba licha ya makato hayo makubwa bado pensheni wanayolipwa kwa mwezi haizidi Sh. 80,000/= na 90,000/=

“Kiasi cha fedha tunacholipwa, hakiendani na hali ya maisha ya sasa. Serikali inapaswa kuangalia namna bora ya kutuongezea pensheni za kila mwezi au baada ya miezi mitatu ili kuendana na hali halisi ya maisha,” amesema Salome Sabula, mmoja kati ya wastaafu hao.

Kwa upande wake mstaafu mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Elizabeth Sylvester amesema, “mimi watoto wangu nimesomesha lakini mpaka sasa baada ya Serikali kusitisha ajira wapo tu nyumbai bado naendelea kuwasomesha wengine, sasa Sh. 80, 000/= tunazolipwa kwa mwezi zitasaidia nini?”

Wamesema kipindi walipostaafu mwaka 1990, walilipwa Sh. milioni 4.4 tu huku walimuomba Rais John Magufuli, kuwaangalia wastaafu wa zamani ili waongezewe fedha ili kukabiliana na makali ya maisha.

Stanslaus Mpembe, Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango amesema lengo la uhakiki wa wastaafu wanaolipwa na wizara hiyo kwenye mikoa mitano ya Kanda ya ziwa unalenga kubaini wastaafu sahihi wanaopaswa kulipwa na serikali.

“Pamoja na kuhakiki wastaafu hao pia tunalenga kuondoa malalamiko na changamoto za wastaafu zilizokuwepo kwa muda mrefu na tunawahimiza wajitokeza kuhakikiwa kabla ya zoezi hilo kukamilika mnamo tarehe 13 Januari mwaka huu,” amesema Mpembe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakazi kwa mawaziri walia majitaka kusambaa mitaani

Spread the loveWAKAZI zaidi ya 4,000 wa mitaa ya Eyasi, TPDC na...

Habari Mchanganyiko

Viumbepori, bahari hatarini kutoweka

Spread the loveKUKOSEKANA juhudi za pamoja za Serikali, wadau wa uhifadhi na...

BiasharaHabari Mchanganyiko

TPSF yataja mbinu ya kuibua vipaji vipya taaluma ya madini

Spread the loveMkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Raphael Maganga...

Habari Mchanganyiko

Kampuni 500 kushiriki maonyesho ya TIMEXPO 2024

Spread the loveSHIRIKISHO la Wenye Viwanda nchini  ( CTI) kwa kushirikiana na...

error: Content is protected !!