July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Wastaafu A. Mashariki hawaidai serikali’

Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima

Spread the love

WIZARA ya Fedha imesema hakuna madai yoyote ambayo Serikali inadaiwa na wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjika.

Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima amelieleza Bunge wakati akijibu swali la Mbunge wa Lindi Mjini, Salum Barwany (CUF).

Barwany alitaka kujua serikali inatoa kauli gani kwa wastaafu hao ambao baadhi yao hawajalipwa kabisa huku wengine wakilipwa kiwango cha chini sana bila kuzingatia hali halisi ya uchumi.

Katika majibu yake, Malima amesema,”wazee hao wamelipwa mafao yao kwa mujibu wa hati ya makubaliano, hakuna madai mengine ambayo serikali inadaiwa.”

Amesema hadi 31 Desemba 2013, serikali imewalipa wastaafu 31,792 ambapo zilitumika Sh. 117 bilioni.

error: Content is protected !!