July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wassira: Msiweke nchi rehani

Baadhi ya watia nia wa nafasi ya Urais kupitia CCM, Edward Lowassa (kulia) akisalimiana na Samuel Sitta

Spread the love

WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, amewataka Watanzania kutoiweka nchi rehani, kwa kuwachagua baadhi ya watangaza nia ya kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wanatumia fedha kuwaraghai ili kukamilisha azma zao. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Wasira alitoa kauli hiyo jana wakati wa harakati za kusaka wadhamini kwenye mkutano uliofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Amesema, Watanzania wanapaswa kuhakikisha wanamchagua kiongozi ambaye hatumii fedha kuwashawishi wamchague.

Wasira ambaye pia ni Mbunge wa Bunda, amesema watanzania wanapaswa kuwa makini na watangaza nia ya urais, kwani wanaotumia fedha wanaweza kuiweka nchi katika umaskini.

Alimesema kuwa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu watajitokeza watu wengi wenye mifuko ya fedha kuwarubuni wananchi, jambo ambalo litaiweka nchi rehani na kusababisha maendeleo kurudi nyuma.

“Rushwa ni kitu kibaya sana na katika kipindi hiki watajitokeza kila aina ya watu wenye pesa kuwarubuni, watanzani ni lazima muwe makini la sivyo mtaiweka nchi reheni,”amesema.

Hata hivyo, amesema endapo atapewa ridhaa na CCM kuongoza nchi kama Rais, atatumia vipaumbele vyake vinne, kupiga hatua kimaendeleo ikilinganishwa na hali ya sasa.

Awali, akitangaza idadi ya wadhamini waliojitokeza kumdhamini waziri huyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela, Loth Ole Lemeirut, amesema walikuwa wanachama 118 kutoka Wilaya ya Nyamagana na Ilemela.

error: Content is protected !!