Saturday , 15 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wasomi wananiangusha – Rais Magufuli
Habari za Siasa

Wasomi wananiangusha – Rais Magufuli

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli ameeleza kusikitishwa na wasomi anaowateua kwenye nafasi mbalimbali kwamba, wengi wao wanamwangusha. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 3 Mei 2019, wakati akihutubia kwenye halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

Kiongozi huyo wan chi ametoa kauli hiyo, baada ya uongozi wa MUST kulalamika kwamba, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imechelewa kutoa hati ya ithibati kwa chuo hicho.

Kufuatia malalamiko hayo, Rais Magufuli ameshangazwa na ucheleweshwaji huo, akisema kwamba, haiwezekani chuo hicho kikose hati ya ithibati wakati watendaji wa mamlaka husika ambao ni TCU iliyochini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknlojia kuna viongozi waliosoma.

“Mi najitahidi kuchagua wasomi nao wananiangusha na wote wako kwenye wizara moja, waziri aliyepo ni profesa, TCU iko chini ya wizara yake, hawa wanalalmika TCU hawatoi waziri upo.

“Sasa natoa siku 10 majibu yawe yametolewa kama ni ndio au hapana, sasa ninaomba waziri shughulikia. TCU washughulikie ithibati mahala pengine wasicheleweshe tunajichelewesha sisi wenyewe,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ametoa siku 10 kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TCU, Profesa Philip Mtabaji pamoja na watendaji kufika chuoni hapo kwa ajili ya kushughulikia changamoto hiyo.

“Mwambie Prof. Mtabaji ndani ya siku 10 awe ameshakuja hapa pamoja na watendaji wake. Ninajua mnanisikia, wajadili kuhusu suala la ithibati.

“Hawezekani changamoto kwamba, TCU huchelewa sana kutoa hati ya ithibati mliomba mpate hiyo hati tangu mwaka 15 aliyepo hapa ni profesa mwenzake anayetakiwa kutoa kibali ni profesa,” amesema Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Mataifa Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/2025 inayolenga kukuza uchumi

Spread the loveMataifa manne ya Afrika Mashariki jana Alhamisi yamewasilisha bungeni bajeti...

Habari za SiasaTangulizi

Gesi asilia, petroli kodi juu

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye...

Habari za SiasaTangulizi

Bilioni 155.4 kugharamia kicheko cha wastaafu 2022-2030

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema jumla ya Sh...

error: Content is protected !!