August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wasimamizi, makarani sensa watakiwa kuwa wazalendo

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla

Spread the love

 

WASIMAMIZI na makarani wote wa sensa yam waka 2022 nchini Tanzania, wametakiwa kutanguliza uzalendo mbele kabla ya mambo mengine. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Ijumaa tarehe 1 Julai, 2022 na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, akifunga mafunzo ya kitaifa ya sensa mkoani Iringa.

“Naomba nisisitize uzalendo uwekwe mbele lolote tutakalokwenda kukabiliana nalo tuweke uzalendo mbele, Utanzania kwanza mengine yatafuata badae,” amesema.

“Naamini mmefurahi kwasababu kwanza mmemaliza mafunzo, na sababu ya pili ni uzalendo wenu wa kuwatumikia watanzania na hili ndiyo jambo kubwa sana.”

Abdulla amesema “sensa hii ina mazoezi mengi ya kitaalamu ambayo kwa utaalamu tumekuwa tukifanya wenyewe na naamini ninyi ni wataalamu wakubwa sana mtatusaidia kufanya kitu chenye historia kwa Tanzania.”

Amesema washiriki wa mafunzo hayo wamepata mafunzo katika ngazi ya Taifa na hivyo kuwa walimu wa walimu katika ngazi za mikoa, wilaya, tarafa, kata na sheia.

“Nimeelezwa kuwa mafunzo haya yamechukua siku 21 kwa kufundishwa kinadharia na kivitendo ni imani yangu kuwa elimu mliyoipata mtaitumia na kuipeleka ipasavyo katika ngazi zingine zinazofuata za mafunzo ili kupata takwimu bora na zinazokidhi vigezo vya kanuni za Umoja wa Mataifa,” amesema Abdulla.

Mkamu huyo wa Rais amesisitiza kamati zote za sensa za mikoa, wilaya, tarafa na sheia kuhakikisha makarani watakaohudhuri mafunzo wawe ni wale wanaojua vizuri maeneo wanayoishi.

“Karani akifahamu vizuri maeneo wanayoishi na watu anaoishi nao itasaidia kuhakikisha wanakaya kuwa na imani ya dhati wakati wa kuchukua taarifa za kitakwimu,” amesema.

error: Content is protected !!