Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Washiriki Miss EA kuanza kambi wiki hii
Tangulizi

Washiriki Miss EA kuanza kambi wiki hii

Spread the love

 

Dar es Salaam. Joto la mashindano ya kimataifa ya urembo ya Miss East Africa 2021 limeanza kupanda ambapo washiriki wa mashindano hayo wataanza kuingia Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Makamu wa Rais wa mashindano hayo, Jolly Mutesi amesema washiriki hao wapo tayari kwa maandalizi ya mwisho ambapo fainali ya mashindano hayo yanayosubiliwa kwa hamu kubwa itafanyika Desemba 17, 2021 katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es salaam

Amesema kwamba msanii Mboso wa Tanzania ni mmoja wa wasanii wakubwa watakaotumbuiza katika mashindano hayo yanayotarajiwa kuangaliwa na mamilioni ya watu barani Afrika LIVE kupitia katika Television na Internet Duniani kote.

Nchi zinazoshiriki mashindano ya Miss East Africa ni pamoja na Kenya, Uganda,
Rwanda, South Sudan na Somalia. zingine ni Reunion, Ethiopia, Malawi, Burundi na Mauritius.

Kiingilio cha chini katika mashindano hayo ni Tsh 50,000 kwa tiketi za kawaida na Sh100,000 kwa VIP na Tsh200,000 kwa VVIP

Mashindano ya Miss east Africa yanaandaliwa na kampuni ya Rena Events kwa kushirikiana na Wasafi Media.

“Tanzania itawakilishwa na Mrembo Queen Mugesi ambae aliwashinda warembo zaidi ya 2,600 wa Tanzania walioomba kuiwakilisha nchi kwa njia ya mtandao ambapo Queen Mugesi alichaguliwa katika mchakato ulioendeshwa na wataalamu wa mambo ya urembo kwa zaidi ya mwezi mmoja,” alisema.

Alisema, mashindano ya Miss East Africa ambayo yaliasisiwa na Mtanzania Rena Callist mwaka 1996, yanasubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa mambo ya urembo na yanatarajiwa kuangaliwa na zaidi ya watu milioni 200

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Makonda kung’oka tena

Spread the loveUWEZEKANO wa Paul Makonda, kuendelea na wadhifa wake wa mkuu...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu: Mabeyo awataje waliotaka kuzuia urais wa Samia

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu...

Habari za SiasaTangulizi

Vilio vyatawala miili ya wanafunzi wanafunzi ikiagwa Arusha

Spread the loveHUZUNI na vilio vimetawala kwa maelfu  ya waombolezaji wakiwemo familia...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Nchimbi aanika ugonjwa wa CCM

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emanuel Nchimbi,...

error: Content is protected !!