Thursday , 13 June 2024
Home Kitengo Biashara Washiriki 600, mifuko 60 kushiriki kongamano la uwezeshaji
Biashara

Washiriki 600, mifuko 60 kushiriki kongamano la uwezeshaji

Spread the love

WADAU 600 na mifuko zaidi ya 60 ya uwezeshaji kutoka sekta za umma na binafsi wanatarajiwa kushiriki kwenye kongamano la saba la uwezeshaji wananchi kiuchumi litafanyika Jijini Dodoma tarehe 29 Septemba mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

 Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa pamoja na Shirika la Care Tanzania na Mfuko wa Fedha wa Self chini ya Wizara ya Fedha, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i  Issa amesema kongamano la mwaka huu litakuwa la kipekee ukilinganisha na yale yaliyopita.

 “Viongozi serikalini wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na makatibu tawala, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa maendeleo wa wilaya wa Mkoa wa Dodoma na jirani, wakuu wa taasisi za serikali na viongozi kutoka sekta binafsi watashiriki kwenye kongomano,” amesema Issa.

 Issa amesema waratibu wote wa uwezeshaji kutoka mikoa yote nchi nzima watakuwepo kwenye kongamano ambalo litaongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambapo ripoti maalum kuhusu uwezeshaji itazinduliwa wakati wa kongamano.

 “Kongamano hili ni muhimu sana katika sekta au tasnia ya uwezeshaji wananchi kiuchumi, kwani ni kipaumbele kikubwa cha serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hasaan,” amesema na kuongeza kuwa kongomano litatanguliwa na maonesho ya wiki ya uwekezaji yatakayoanza Septemba 26 hadi 28.

 Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara na Masoko wa Mfuko wa Fedha wa Self kutoka Wizara ya Fedha, Petro Mattaba amesema mfuko huo unafanya kazi karibu sana na Baraza la Uwezeshaji na mpaka sasa Watanzania 240,000 wameshanufaika mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 228.

“Tuna matawi kwenye mikoa 12 ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Shinyanga, Geita, Tanaga, Mbeya, Mwanza kwa uchache wake. Tunatoa mikopo, kuzijengea uwezo taasisi za fedha na kutoa elimu ya masuala ya fedha,” amesema 

Mattaba amewaomba Watanzania kujitokeza kwenye maonesho ya uwekezaji ili waweze kujifunza mbinu mbalimbali.

Amesema wanufaika wakubwa wa mikopo ya Self ni wanawake, vijana na makundi maalumu na kwamba mfuko huo kupita NEEC utawafikia Watanzania wengi na kufikia matarajio aliyonayo Rais Samia.

 Naye Mkurugenzi wa Miradi wa Care Tanzania, Haika Mtui amesema shirika lake limekuwa likiunga mkono juhudi za serikali za kuwaondoa wananchi kwenye wimbi la umaskini na hasa kuwajengea uwezo.

“Tangu shirika lianzishwe mwaka 1994, zaidi ya wananchi 800,000 kati yao asilimia 70 ni wanawake. Tunaunga mkono juhudi za serikali katika kubadilisha maisha ya wanawake na vijana,” amesema na kuwataka Watanzania kuchangamkia fursa zinazotolewa na NEEC kwa kushirikiana na wadau wake.

 Kauli Mbiu ya Kongamano hilo la saba ni ‘Uwezeshaji kwa Uchumi Endelevu’ kwani inatoa fursa ya kujadili kwa kina masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa uchumi endelevu wa Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Prof. Mkumbo: Pato la taifa limefikia trilioni 148

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema mwaka...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Deni la Serikali lafikia trilioni 91

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema hadi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

GGML yaahidi kuendelea kushirikiana na UDSM kudhamini tafiti, ubunifu

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imeahidi kuendelea kushirikiana...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Marekani yasaka fursa uwekezaji sekta ya nishati Tanzania

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko amekutana...

error: Content is protected !!