June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Washindi wa M Bet wakabidhiwa vitita vyao

Spread the love

WASHINDI wawili, Exaudi Mgeni wa Iringa na Joel Mwakagali wa Mbeya, waliojinyakulia jumla ya kitita cha Sh. 82 milioni, wamekabidhiwa fedha zao leo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Abbas Tarimba, Mkurugenzi wa Bosi ya Bahati Nasibu ya Taifa, anaandika Mwandishi wetu.

Akizungumza kabla ya kukabidhi mfano ya hundi yenye thamani ya fedha hizo, Tarimba ameipongeza M-Bet kwa kuendesha mchezo huo kwa ufanisi, lakini pia washindi hao kwa kuibuka kidedea.

Amesema, bodi yake inafarijika kuona washindi hao wakiliingizia pato Taifa kupitia kodi watakayolipa kwa kushinda fedha hizo ambazo ni kama Sh 7 milioni huku akiwataka kuhakikisha wanazitumia ipasavyo fedha hizo kuboresha maisha yao.

“Michezo ya –ku-bet’ tumeweza kuilea ili kutoa nafasi kwa wanamichezo kushiriki michezo hii ya kubahatisha ambayo ni neema kwa taifa na si janga kama baadhi ya watu wanavyodhani,” amesema Tarimba.
Amesema, kwa kuonesha jinsi michezo hiyo ilivyo na tija kwa taifa, mwaka 2014-15, ililiongezea taifa pato la Sh 15 milioni kupitia kodi, wakati mwaka uliofuata, iliingiza kiasi cha Sh 240bilioni.

Dhiresh Kaba, Mkurugenzi wa M-Bet amesema kuwa, Mgeni na Mwakagali, walifanikiwa kuzoa kitita hicho baada ya kufanikiwa kutabiri matokeo ya mechi 12 za ligi za Ulaya kwa Super 12.

“Tunafarijika kuwakabidhi kitita chao cha Sh milioni 82 Joel na Exaudi kama washindi wa m-Bet ambao kila mmoja atapata Sh milioni 41 kabla ya makato ya kodi,” amesema Kaba.

Amewataka watanzania kuchangamkia kutumia mtandao wa intaneti kuonesha ushabiki halisi wa soka akisema kuwa Super 12 ni mchezo wa ziada unaoruhusu kutabiri mechi 12 kwa Tsh 1,000 tu ambapo ukipatia zote kama Mgeni na Mwakagali, unaondoka na kikapu cha siku.

 

error: Content is protected !!