Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Washindi NMB MastaBata ‘Kote Kote’ wapaa Dubai
Habari Mchanganyiko

Washindi NMB MastaBata ‘Kote Kote’ wapaa Dubai

Spread the love

WASHINDI saba wa kampeni ya kuhamasisha matumizi ya kadi iliyoondeshwa na Benki ya NMB ‘NMB MastaBata – Kote Kote’ wameagwa na kukabidhiwa tiketi za safari yao ya Dubai iliyolipiwa gharama zote, na tayari wameondoka nchini jana mchana. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hafla ya makabidhiano na kuwaaga washindi hao na wenza wao, imefanyika leo tarehe 28 Februari 2023 Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam, ambapo walikabidhiwa tiketi zao na Mkuu wa Idara ya Kadi ya NMB, Philbert Casmir.

Mkuu wa Idara ya Kadi Benki ya NMB, Philbert Casmir (kushoto) akimkabidhi mfano wa tiketi ya ndege mmoja wa washindi wa safari ya kwenda Dubai wa Kampeni ya NMB Mastabata Kote Kote, Rose Qamara wakati wa hafla ya kuwaaga washindi saba na wenza wao iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Biashara Benki ya NMB, Alex Mgeni, Mkuu wa Idara ya Wateja Maalum, Getrude Mallya (wa pili kulia) na kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Kadi, David Ngusa.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Casmir alisema kwamba malengo matatu ya kampeni hiyo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa, huku akiyataja kuwa ni pamoja na kuhamasisha matumizi ya kadi, ambayo ni rahisi, nafuu na salama zaidi, kuliko matumizi ya pesa taslimu, ambayo ni hatarishi na ya gharama kubwa.

 “Malengo mengine ya NMB MastaBata yalikuwa ni kurejesha kwa wateja sehemu ya faida jambo linalothibitisha namna tunavyowajali, lakini pia kampeni ililenga kuthibitisha uimara wetu katika masuluhisho ya kidijitali, ambako NMB tumefanya uwekezaji mkubwa.


Mkuu wa Idara ya Kadi Benki ya NMB, Philbert Casmir (wa pili kushoto) akimkabidhi mfano wa tiketi ya ndege mmoja wa washindi wa safari ya kwenda Dubai wa Kampeni ya NMB Mastabata Kote Kote, Upendo Msanjila, wakati wa wa hafla ya kuwaaga washindi saba na wenza wao iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Biashara Benki ya NMB, Alex Mgeni, Mkuu wa Idara ya Wateja Maalum, Getrude Mallya (wa pili kulia) na kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Kadi, David Ngusa.

“Katika hili, NMB tumeshirikiana na MasterCard na tunawatakia washindi wetu ambao wataongozana na maafisa wa benki yetu safari njema, ambayo tunaamini itakuwa na siku nne zenye mambo mengi ya kujifunza, ikiwemo fursa za kibiashara na utalii,” alisema Casmir.

Aliongeza ya kwamba, mwisho wa NMB MastaBata ‘Kote Kote’ iliyoanza Oktoba 28 mwaka jana, ni mwanzo wa kampeni nyingine mbalimbali, huku akiwataka Watanzania na wateja wa NMB kukaa mkao wa kuchangamkia kila fursa inayokuja kupitia huduma za benki hiyo.

Washindi na wafanyakazi wawili waliokabidhiwa tiketi na kuondoka jana mchana ni pamoja na Rose Qamara, Upendo Msanjila, Edwin Mwakabage, Nazia Lakha, Xaveria Hyera,  Chintan Kamania na John Lubisha.

Akizungumza kwa niaba washindi hao, Upendo Msanjila alikiri kufurahishwa sana na safari hiyo, ambayo awali wakati akipigiwa simu ya ushindi hakuamini akihisi ni matapeli na kwamba NMB imewezesha kwa mara ya kwanza yeye kutembelea Dubai akiwa na mwenza wake.

Naye John Lubisha, alielezea kiwango cha juu cha furaha yake kwa kushinda moja kati ya nafasi saba zilizokuwa zikishindaniwa na wateja zaidi ya Milioni 5 benki hiyo katika kipindi cha miezi mitatu iliyojumuisha zawadi zenye thamani ya zaidi ya Sh. Mil. 350.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!