Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Washindi NMB MastaBata Kote-Kote wafikia 608
Habari Mchanganyiko

Washindi NMB MastaBata Kote-Kote wafikia 608

Spread the love

IDADI ya washindi wa kila wiki wa kampeni ya NMB MastaBata Kote-Kote sasa imefikia 608 baada jana Ijumaa, tarehe 13 Januari 2023 kupatikana washindi wa raundi ya nane ya droo za kila wiki hapa Mtwara ambapo zawadi zenye thamani ya takribani 10m/- zilinyakuliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwenye droo hiyo iliyofanyika katika Tawi la NMB Mtwara, wateja 76 wa benki hiyo kiongozi na kinara wa fedha kidijitali nchini Tanzania walishinda pesa taslimu na pikipiki moja zinazotolewa kila wiki.

Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Kusini Janeth Shango (kushoto) akimkabidhi pikipiki mshindi wa Pikipiki katika droo ya NMB Mastabata kote-kote, Husna Juma Baraka kutokea Mtwara. Kulia ni Meneja wa huduma kwa wateja wa Benki ya NMB tawi la Mtwara, Mohamed Fundi. Benki ya NMB imeshatoa Pikipiki kumi na moja mpaka sasa zikiwa ni zawadi kwa wateja wa NMB wanaofanya malipo kupita NMB mastercard au Mastercard QR katika msimu huu wa Mastabata.

Akizungumza kabla ya zoezi la kuwapata washindi hao, Meneja wa NMB Kanda ya Kusini, Janetrh Shango, alisema 75 watapata 100,000/- kila mmoja na mwingine kunyakua pikipiki aina ya Boxer.

Kwenye droo saba za kila wiki zilizotangulia, washindi 525 walishinda fedha taslimu zenye thamani ya 52.5m/- huku saba kila mmoja akishinda Boxer ambazo zote thamani yake sokoni sasa hivi ni kama 21m/-..

“Lengo la msingi la kampeni hii ya MastaBata Kote-Kote, kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake, ni kuhamasisha na kuwashawishi wateja wetu kutumia kadi za NMB Mastercard na NMB Mastercard QR wanapofanya malipo na wanaponunua bidhaa na huduma mtandaoni au kwenye vituo vya malipo,” alisema Shango.

Aidha, alisema promosheni za malipo kidijitali za NMB MastaBata zinatumika kuwalipa fadhila wateja wao waaminifu and kama sehemu ya kutekeleza sera ya benki hiyo ya kurudisha kiasi fulani cha faida kwa jamii.

Mchakato wa kampeni za MastaBata ulizinduliwa mwaka 2018 kwa lengo kuu la kuhamasisha matumizi ya kadi za malipo za NMB sambamba na ajenda ya taifa ya fedha kidijitali ambayo inalenga kupunguza matumizi ya fedha taslimu na kuifanya Tanzania nchi ya uchumi wa kisasa wa kidijitali.

Shango alisema awamu hii ya nne ya kampeni ya NMB MastaBata ilizinduliwa tarehe 28 Oktoba mwaka jana na itatamatika mwezi huu.

Mbali ya droo za kila wiki ambazo mpaka sasa washindi 608 wameshinda zawadi zenye thamani ya kama 84m/-, shindano hili pia limehusisha droo mbili za kila mwezi ambapo washindi 98 wamenyakua 1m/- kila mmoja huku wanne wakishinda Boxer kila mmoja wao.

Thamani ya zawadi za kila mwezi zilizonyakuliwa na washindi 102 ni kiasi cha kama 110m/-. Thamani ya zawadi zote za MastaBata Kote-Kote ni zaidi ya 300m/-.

Kampeni ya NMB MastaBata Kote-Kote inatarajiwa kuhitimika kabla ya mwisho wa mwezi huu kwa kufanyika droo kubwa ya mwisho ambapo washindi saba watashinda zawadi ya safari ya mapumziko ya siku nne huko Dubai wakiwa na wenza wao.

Kwenye droo ya jana, mshindi wa Boxer wa raundi ya saba, Husna Juma Baraka, ambaye ni askari polisi wa Mtwara, alikabidhiwa zawadi yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!