Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Michezo Washindi NBC Jaza Kibubu Tusepe Qatar Wakwea ‘Pipa’ Kuishuhudia Uingireza na Ufaransa
Michezo

Washindi NBC Jaza Kibubu Tusepe Qatar Wakwea ‘Pipa’ Kuishuhudia Uingireza na Ufaransa

Spread the love

YAMETIMIA! Hatimaye washindi wa wanne wa kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar inayoendeshwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wameanza safari  jana tarehe 8 Disemba, 2022 kuelekea nchini Qatar kushuhudia mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 kati ya Uingereza na Ufaransa itayochezwa Disemba 10, mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Washindi hao wannne Abdallah Tangarisi (Singida), Victor George Mwaifunga (Dar es salaam), Konolia Leonard Hinju (Songea) na Mpoki Wamakimbika (Mbeya) wameondoka jijini Dar es Salaam jana mchana wakiambatana na baadhi ya maofisa kutoka benki ya NBC.

Maofisa wa benki ya NBC akiwemo Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Kimaryo (kushoto) na Meneja Biashara na Mauzo wa benki hiyo, Dorothea  Mabonye (Kulia) sambamba na washindi wa kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar inayoendeshwa na benki hiyo wakionesha nyaraka za kusafiria muda mfupi kabla kuanza safari kuelekea nchini Qatar kushuhudia mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 kati ya Uingereza na Ufaransa itayochezwa Disemba 10, mwaka huu. Hafla ya kuwaaga washindi hao imefanyika jijini Dar es Salaam jana.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza kwa safari hiyo, Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Kimaryo alisema wakiwa nchini Qatar washindi hao watapata fursa ya kwenda uwanjani ili kushuhudia mechi ya robo fainali ya michuano hiyo kati ya mataifa mawili vinara kwenye mchezo wa soka, Uingereza na Ufaransa.

“Hatimaye maandalizi ya safari ya kuelekea Qatar sambamba na washindi wetu wa kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar yamesha kamilika na sasa tupo tayari kupanda ndege kuelekea huko kutazama mechi ya robo fainali baina ya Ufaransa na Uingereza. Benki ya NBC tutagharamia gharama zote kuanzia usafiri wa kutoka hapa kwenda Qatar, malazi na gharama zote zitakazohusika katika safari yote huko Qatar” alisema Alina.

Mkurugenzi wa wateja Wadogo wa NBC,Bw  Elibariki Masuke (kulia) akizungumza na washindi wa kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar inayoendeshwa na benki hiyo muda mfupi kabla kuanza safari kuelekea nchini Qatar kushuhudia mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 kati ya Uingereza na Ufaransa itayochezwa Disemba 10, mwaka huu. Hafla ya kuwaaga washindi hao imefanyika jijini Dar es Salaam jana.

Kwa mujibu wa Alina, wakiwa huko pamoja na kutazama mechi hiyo washindi hao watapata fursa nzuri ya kutembelea maeneo mbalimbali yenye mvuto ikiwa ni sehemu ya utalii, hatua ambayo itaongeza radha ya safari hiyo kwa washindi hao.

“Lengo letu ni kuhakikisha washindi wetu wanafurahia siku watakazokuwa huko na ndio maana tutao fursa kwao kuweza kutembelea maeneo yenye mvuto zaidi wakiwa huko ili waweze kufanya utalii pia,’’ aliongeza.

Kabla ya kuanza safari hiyo, washindi hao walipokelewa rasmi jijini Dar es Salaam jana na wenyeji wao benki ya NBC na kutambulishwa rasmi katika hafla fupi ya jioni iliyohudhuliwa na wadau mbalimbali wa mchezo wa soka nchini sambamba na maofisa  wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa wateja Wadogo wa NBC,Bw  Elibariki Masuke.

Mkurugenzi wa Hazina na Masoko Benki ya NBC,Bw Peter Nalitolela   (wa pili kulia) akizungumza na washindi wa kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar inayoendeshwa na benki hiyo muda mfupi kabla kuanza safari kuelekea nchini Qatar kushuhudia mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 kati ya Uingereza na Ufaransa itayochezwa Disemba 10, mwaka huu. Hafla ya kuwaaga washindi hao imefanyika jijini Dar es Salaam jana.

Wakielezea hisia zao kufutia ushindi wao na safari hiyo, washindi hao walisema imekuwa ni furaha kubwa kwao kwa kuwa hawakutarajia safari hiyo, huku wakiipongeza benki ya NBC kwa kampeni hiyo iliyowawezesha kwenda nchini Qatar kushuhudia mchezo wanaoupenda wakiwa wamelipiwa kila kitu.

“Iliniwia vigumu kuamini kwamba nimeshinda safari hii hadi pale nilipothibitishiwa na maofisa wa benki ya NBC tawi la Mbeya. Nimekuwa mteja wa NBC kwa muda mrefu na nimekuwa nikifurahia huduma zao muda wote ila kwa hili wamenifurahisha sana na ninaahidi kuendelea kuwa balozi mkubwa wa benki hii…nawashukuru sana benki ya NBC,’’ alisema Bi Mpoki Wamakimbika mshindi wa kampeni hiyo kutoka Mbeya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!