Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Washereheshaji wawakumbuka watoto yatima, wafungwa
Habari Mchanganyiko

Washereheshaji wawakumbuka watoto yatima, wafungwa

Spread the love

MARAFIKI wa Mshehereshaji (MC) Mwangata Fomma wametoa msaada kwa kuwalipia kadi za bima ya afya kwa watoto nane wa Kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu na yatima cha Masisita wa Mt. Urusula kilichopo Miyuji Jijini Dodoma.

Pia wametoa msaada wa magodoro 20 kwa wafungwa wa Gereza la Isanga ambapo magodoro 10 watapewa wafungwa wanawake na 10 watapewa wafungwa wanaume. Anaripoti Danson Kaijage …(endelea).

Msaada huo umetolewa leo tarehe 19 Machi, 2022 na kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha mwaka mmoja aliotimiza akiwa madarakani.

Akizungumzia msaada huo mmoja wa marafiki hao wa MC Mwangata, Naterius Lukinjason amesema umoja huo pia umetoa misaada ya sukari, mafuta ya kupaka kwa watoto hao wa kituo hicho cha kulelea watoto.

Aidha, akitoa neno la shukrani Msaidizi wa kituo, Sista Elizabeth Mtema amewashukuru wana umoja huo kwa kuona umuhimu wa kutoa sadaka kwa watoto hao.

“Kwa niaba ya mkuu wa kituo hiki Alizea Kyara, nipende kuwashukuru kuwapatia baadhi ya watoto bima za afya na misaada mingine ya chakula na mafuta.

“Kituo kina jumla ya watoto 62 na kwa sasa wapo watoto 36 kwa kuwa wapo watoto ambao wapo katika vyuo mbalimbali,” amesema.

Aidha, amesema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa chakula baada ya wafadhili kuzeeka pamoja na kushuka kwa uchumi kutokana na kuwepo kwa changamoto ya ugonjwa wa uviko-19.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!