February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wasanii wapewa neno kuondokana na aibu

Jimmy Mafufu, Makamu  Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania

Spread the love

MAKAMU  mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania, Jimmy Mafufu amewataka wasanii kujiunga katika mfumo wa bima kupitia mfuko wa PPF ili kuondokana na aibu za kuchangishana fedha kupitia vyombo vya habari wakati wa matatizo, anaandika Hamis Mguta.

Mafufu amesema kuwa lengo la mfuko wa PPF ni kusaidia watanzania, lakini wameona wasanii pia wana matatizo mengi.

“Watu hawana bima za afya, wanaumwa wanachangishana kwenye TV, ni aibu sana kuona msanii anaumwa harafu Radio, Magazeti na TV zinaandika achangishiwe pesa,” amesema Mafufu.

Amesema kuwa tarehe 14 Octoba mwaka huu, waigizaji, waaandaaji wa filamu wadau na watanzania wote watatakiwa kufika katika viwanja vya posta jijini Dar es Salaam ili kujiunga katika mfuko huo.

“Kupitia PPF waigizaji tunakwenda kupata sifa za kukopesheka na dhamana yako ni mchango uliochangia tu, kujiunga ni hure lakini kila mwisho wa mwezi mtu ambaye anajiunga atalipa Sh 20,000,” amesema.

Mtazame kwenye video hii…

error: Content is protected !!