Thursday , 13 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Wasanii wamvaa Sirro kumdai Roma
Habari MchanganyikoMichezoTangulizi

Wasanii wamvaa Sirro kumdai Roma

Ibrahim Mussa 'Roma'. Picha ndogo kulia, msanii Moni na kushoto ni Kamanda Simon Sirro
Spread the love

NI siku ya pili tangu msanii wa muziki wa Hip-Hop, Ibrahim Mussa ‘Roma’ na wenzake kukamatwa na watu wasiojulikana katika Studio za Tongwe Records, anaandika Hamisi Mguta.

Kufuatia tukio hilo wasanii wa muziki wameungana kuwatafuta wasanii wenzao ambao taarifa zao hazifahamiki hata katika vyombo vya usalama.

Wakizungumza na waandishi wasanii hao wakiongozwa na Mke wa Msanii huyo, Mama Ivan, Farid Kubanda ‘Fid Q’, Mrisho Mpoto, Kala Jeremah, Junior Makame ‘J Mada’ ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tongwe na wengine wamesema wanafanya jitihada za kumtafuta kwa kuomba msaada kwa polisi.

Katibu wa shirikisho la wasanii aliyetambulika kwa jina la Briton amesema wamejaribu kuzunguka vituo vya polisi vyote vikubwa vya karibu na tukio lilipotokea lakini hakuna matokeo mazuri.

“Nimezungumza na Kamanda wa Polisi wa Dar es Salaam, Simon Sirro na yeye amesisitiza kuwa tuendelee kuwa na uvumilivu ili wafanye uchunguzi suala hilo na kupunguza munkali ya kuilaumu serikali,” amesema Briton.

Briton amesema kama wasanii hawailaumu serikali hata kidogo bali wanajaribu kupaza sauti ili kuomba, kutetea kulinda usalama wa wasanii wanzao.

“Kamanda Sirro ametuahidi kesho saa tano tufike ofisini kwake kwa ajili ya kupata taarifa zitakazopatikana,” amesema.

Akielezezea namna tukio hilo lilivyotokea Mkurugenzi wa Tongwe, Junior Makame amesema Aprili 5, 2017 majira ya saa moja jioni ilikuja gari aina ya Noah katika maeneo ya studio hiyo na inasemekana walikuwa watu watano ambao wote walikuwa wanaume na kumuulizia yeye pamoja na Roma.

“Mimi sikuwepo kulikua alikuwepo Moni ambaye ni msanii wa tongwe, ‘producer’ wetu mwengine anaitwa Bin Laden na Ima ambaye ni houseboy wa mama yangu,” amesema Makame.

Amesema kwa kuwa hakuwepo taarifa hizo alipatiwa na msanii mwenzao anaitwa ‘The City’ ambaye alishuhudia tukio wakati anaingia katika eneo hilo.

Makame amesema kuwa ilipofika saa saba hawakupata matumaini yoyote, ndipo akaamua kupiga simu kwa mke wa Roma kumueleza kilichotokokea.

Alipohitajika kuzungumza Mke wa Msanii Roma alishindwa kumaliza maelezo na kuangua kilio dakika chache baada ya kuanza kujieleza.

“Sina cha kusema zaidi, lakini nilipata taarifa usiku wa saa sita, nilipigiwa simu kwa kifupi naomba msaada wenu waandishi pamoja na polisi,” amesema Mama Ivan huku akilia.

Kesi kuhusu kukamatwa kwa wasanii hao imefunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tongwe katika kituo cha Polisi Oysterbay RB namba OB/RB/5272/017.

Naye msanii Mrisho Mpoto amesema tukio hilo si jambo la kawaida kutokea nchini, ukilinganisha na siku zilizopita hasa katika tasnia ya sanaa.

“Tunaomba tuungane katika kuwatafuta kina Roma, kwa kutuma ujumbe ama taarifa kuhusu wasanii hao kwa kutumia hashtag ya AkinaRomaWakoWapi katika mitandao ya kijamii, (#AkinaRomaWakoWapi).

Msanii mwengine Kala Jelemaya ameviomba vyombo vya usalama viendelee kusaidia kutafuta na kutatua suala hili kwa kuwa halioneshi picha nzuri kwa taifa.

“Nimewasiliana naye usiku wa siku aliyokamatwa, nilikaa naye Lion Hoteli siku hiyo kabla ya kukamatwa, tunaomba vyombo vya ulinzi vitusaidie,” amesema Kala.

Hata hivyo Msanii Kala Jeremah ametoa wito kwa wasanii wengine kuendelea kupaza sauti kwa sababu hakuna njia nyingine na kuwa serikali inapaswa kujua kuna vijana tumejiajili kupitia sanaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Deni la Serikali lafikia trilioni 91

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Mbunge Dk. Shogo Mlozi afariki dunia

Spread the loveMbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ambaye pia ni...

BiasharaHabari Mchanganyiko

GGML yaahidi kuendelea kushirikiana na UDSM kudhamini tafiti, ubunifu

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imeahidi kuendelea kushirikiana...

KimataifaTangulizi

Boti yazama DRC, 80 wafariki dunia

Spread the loveJUMLA ya watu 80 wameripotiwa kufariki dunia huko nchini Congo...

error: Content is protected !!