January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wasanii chipukizi waomba ushirikiano kwa wakongwe

Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Vijana Arts Group wakiwa katika picha ya pamoja

Spread the love

WADAU wa sekta ya Sanaa nchini Tanzania wametakiwa kuungana na kushirikiana katika kazi zao ili kuleta ushindani kwa nchi za jirani katika tasnia hiyo ya sanaa.

Rai hiyo ilitolewa jana na mkurugenzi wa Kikundi cha Vijana Arts Group kilichopo Kinondoni maeneo ya ukumbi wa Vijana, likiwa chini ya uongozi wa vijana watatu Alhad Kakwaya, Abdulmajid Kimwaga na Awax.

Akizungumza na MwanaHALISI Online mmoja kati ya wakurugenzi hao, Kakwaya, kuwa kundi hilo lilianzishwa April 2 mwaka jana likiwa na washiriki kumi ambao tayari walikuwa wameshapitia makundi mengi ya sanaa na kukata tamaa kabisa.

Kakwaya alisema waliamua kuazisha kundi hilo la sanaa ambalo linafanya kazi mbalimbali ikiwemo sanaa ya maigizo, muziki, kuandaa vipindi vya televisheni na redio pamoja na matangazo.

Alisema lengo la kuazisha kundi hilo ili kuweza kupunguza kundi la vijana mitaani, waliokata tamaa ya maisha na kuweza kujiajili wao wenyewe kwa kutumia vipaji vyao.

“Changamoto tunayopata wasanii wachanga ni kukosa nafasi ya kutoa mchango wetu wa kimawazo kuhusiana na sanaa, kutengwa na wasanii wakubwa, hatupati haki zetu za msingi kutoka kwa makampuni yanayonunua kazi zetu hawapokei kazi zetu kadi awepo msanii mkubwa,’ alisema Kakwaya.

Aidha Kakwaya aliongeza, matarajio yao makubwa ni kuwa na kampuni yao binafsi na kuwa na vifaa nyote vinavyohusiana na uzalishaji wa kazi zao ili kupunguza gharama ambazo wanazipata kwa sasa na badala yake kuongeza mtaji kwajili ya maendeleo ya vijana.

Habari hii imeandikwa na Sarafina Lidwino 

error: Content is protected !!