Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Wasambazaji, wauzaji dawa ya Gentrisone wakamatwa
Afya

Wasambazaji, wauzaji dawa ya Gentrisone wakamatwa

Dawa ya Gentrisone
Spread the love

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), imeondoa sokoni dawa bandia aina ya Gentrisone 10g Cream, zaidi ya tube 4,188. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 17 Julai 2019 kwa umma na TMDA, inaeleza kwamba dawa hizo zilibainika katika zoezi la ukaguzi wa masoko ya dawa, ililofanya kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa, katika Mkoa wa Mwanza zilizondolewa tube 1,814, Dar es Salaam (931), Mtwara (817), Dodoma (591), Tabora (29) na Arusha (6)

“Watuhumiwa wote mbalimbali wamekamatwa ikiwa pamoja na mwendesha pikipiki aliyehusika katika kusambaza dawa hii kwenye maduka binafsi na rejareja ambaye analisaidiaa polisi kufahamu mtandao.,” inaeleza sehemu ya taarifa ya TMDA.

TMDA imeeleza kuwa, dawa hiyo iliyotengenezwa na Kiwanda cha Shin Poong Pharm Co. Ltd kilichopo Jamhuri ya Korea na kusambazwa nchini na Kampuni ya K&C Trading Co. Ltd ya Dar, imefanana na dawa halisi ya Gentrisone 10g Cream.

“Dawa bandia inaonesha kwenye lebo namba ya toleo (GNTRO X030) iliyotenenezwa tarehe 21 Aprili 2019 na kuisha muda wa matumizi tarehe 20 Aprili 2022 na namba ya usajili TAN00.368 D07C SHI, dawa hii kwa kiasi kikubwa imefanana na dawa halisi ambapo utofauti wake ni kwenye namba ya tokeo na mtengenezaji amethibitisha hajawahi kutengeneza toleo hilo,”

TMDA imesema kutokana na kuwepo kwa dawa bandia na kwa mujibu wa utaratibu, mtengenezaji na msambazaji wameelekezwa kushirikiana na mamlaka hiyo kuondoa matoleo yote kwenye soko ambayo ni bandia ili wananchi wasiendelee kununua.

Aidha, mamlaka hiyo imetoa agizo kwa wauzaji wote wa dawa nchini kama wana dawa hiyo katika stoo au maghala yao, kuacha kuzisambaza mara moja, na wasiliane na TMDA ili kupewa utaratibu wa wapi pa kuzipeleka.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!