July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Wasaka urais CCM walaghai’

Mtangaza nia Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Nyamagama, Ezekiel Wenje

Spread the love

MBUNGE wa Jimbo la Nyamagana, Mkoa wa Mwanza (Chadema), Ezekiel Wenje amesema, wasaka Urais ndani ya CCM ni walaghai kwa kuwa, hawana sifa na vigezo vya kuwatumikia wananchi. Anaandika Moses Mseti … (endelea).

Amesema, watangaza nia hao hawana sifa, vigezo na uwezo kutumikia wananchi kwa kuwa, wameshindwa kuongoza na kusimamia wizara zao na kusababisha nchi kuingia katika janga la umaskini.

Kauli hiyo aliitoa jazi wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake, Wilaya ya Nyamagana ambapo amesema, umefika wakati Watanzania wakawakimbia watia nia hao kwa kuwa ni walaghai.

Wenje aliwataja baadhi ya watangazania nia hao ambao walishindwa kuongoza wizara zao ni Mawaziri wakuu wa Zamani, Fredrick Sumaye na Edward Lowasa; Waziri wa Kilimo na Ushirika, Steven Wassira kwamba hawana sifa za kuongoza kwani tangu enzi za Mwalimu Julias Nyerere, walikuwepo.

“Nawashangaa sana hawa watangaza nia wa CCM, wakati wakiwa serikalini walishindwa kuwatumikia na kutumia hivyo vipaumbele vyao, iweje sasa hivi wanakuja na mikakati ambayo hataweza kuitekeleza.

“Wengine mpaka sasa hivi ni viongozi na wameshikilia wizara nyeti, wameshindwa kuwatumikia, akiwemo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mbona sasa hivi hajafanya chochote anasubiri nini?” amehoji.

Hata hivyo amesema, mwarobaini wa kuwakomboa Watanzania kutoka katika janga hili la umaskini na mtu pekee wa kubadilisha maisha ya Watanzania ni Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Amesema, endapo Watanzania wataamka na kuachana na matapeli wa CCM na kukiunga mkono kwa kukichagua Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, janga la njaa na ajira itakuwa mwisho.

Katibu Raslimali watu Chadema Kanda ya Ziwa Victoria, Lina Kavet amesema, CCM imeshindwa kuwawezesha wanawake na kusababisha wakina mama kuendelea kuuza matunda na dagaa.

Amesema, umefika wakati Watanzanaia kukombolewa na kutoka katika mateso ya CCM, ambao wamewafanya Watanzania kama wajinga na wao kuendelea kutumia raslimali za taifa hili.

error: Content is protected !!