December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wasafi FM yafungiwa siku 7

Spread the love

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kusitisha utoaji huduma za utangazaji kwa Wasafi FM kwa muda wa siku saba baada ya kukiuka kanuni za utangazaji kwa kutumia lugha za matusi kwenye kipindi cha The Switch na Mashamsham. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa tarehe 11 Septemba 2020 jijini Dar es Salaam, amewataka Wasafi FM kutumia siku nzima ya leo kuomba radhi kutokana na ukiukwaji huo wa kanuni kwa kutumia lugha za matusi ambazo hazikubariki.

Kilaba amesema, adhabu hiyo itaanza kutumika kesho Jumamosi tarehe 12 hadi 18 Septemba 2020 na endapo Wasafi FM hawatatekeleza adhabu hiyo, TCRA itachukua hatua kali zaidi.

James Kilaba, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Mkurugenzi mkuu huyo, ametoa wito kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kutumika kuonyana ili kunusuru adhabu hizo ambazo hawapendi kuzitoa.

Adhabu ambayo wameipata Wasafi FM inafanana na walioipta Clouds Televisheni na Clouds Redio ambazo TCRA iliifungia kwa siku saba kuanzia tarehe 28 Agosti hadi 3 Septemba 2020

Pia, TCRA ilitaka Clouds kutumia vituo vyake kuomba radhi tarehe 27 Agosti 2020 kutokana na ukiukwaji wa kanuni za utangazaji kupitia kipindi cha Clouds 360.

error: Content is protected !!