June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Warioba ainyooshea kidole Takukuru, Rais Magufuli…

Jaji,Joseph Warioba Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba

Spread the love

WAZIRI Mkuu mstaafu wa Tanzania, Joseph Sinde Warioba amesema, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inapaswa kuachwaa ili itekeleze wajibu wake pasina kuingiliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea)

Pia, Warioba aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba amesema, Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli anahitaji msaada mkubwa ili kuendesha mapambano dhidi ya rushwa.

Warioba ambaye ni Jaji mstafau amesema hayo leo Jumatatu tarehe 24 Agosti 2020 wakati akifungua kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere lililofanyikia Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kivukoni jijini Dar es Salaam.

Amesema enzi za uhai na maisha yote ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Mwnyerere aliyefariki dunia 14 Oktoba 1999 London nchini Uingereza, alipambana na rushwa, hakupokea wala kutoa rushwa.

Rais John Magufuli

Jaji Warioba amesema, ajenda ya Rais Magufuli ya kulinda rasilimali kwa kupiga vita rushwa ni kazi kubwa na Rais anahitaji msaada ili kurudisha nidhamu kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla.

“Rushwa bado ipo kwenye maeneo mbalimbali rushwa ipo kwenye vyama vya siasa, ipo kwenye vyama vya michezo na rushwa ipo kwenye taasisi nyingine za serikali,” amesema Jaji Warioba huku akishangiliwa na washiriki wa kongamano hilo

Jaji Warioba amesema, wakati wa uchaguzi, vyama vya siasa vimetoa onyo wasitoe rushwa lakini kwenye mchakato wa uteuzi wameshuhudia rushwa ikitembea.

“Tujiulize ni nani walioongwa kwenye uteuzi, utakuta ni viongozi, kwa kuwa kwenye mikutano ya uteuzi, wajumbe wake ni viongozi kuanzia kata hadi Halmashauri,” amesema.

Amesema, hawawezi kumaliza rushwa mpaka wananchi waikatae na kuikataa mpaka viongozi washawishi.

“Rais Magufuli anahitaji msaada mkubwa ili tufike mahali wananchi wakubali na viongozi wasijidumbukize katika rushwa. Ajenda ya Rais ya kupambana na rushwa ni nzuri lakini hali ya kupambana nayo siyo nzuri sana,” amesema.

“Nina wasiwasi na Takukuru kwa sababu ipo chini ya viongozi, haitafanya kazi yake vizuri, ninadhani iwe huru ifanye kazi yake bila kufuata maagizo ya viongozi yeyote la sivyo itakuwa sehemu ya utawala na kupewa maagizo na serikali,” amesema.

Ludovick Utouh, Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu

Kwa upande wake, aliyewahi kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema, kumekuwa na mazingira tofauti ya utoaji rushwa ambayo yameendelea katika jamii.

Utouh amesema, mwaka huu ni wa uchaguzi na kama wakichanguliwa viongozi waliotoa rushwa pindi wakiingia madarakani wanakwenda kupambana kujirudishia fedha zao sio kufanya kazi hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini.

Awali, Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila amesema, lengo la kongamano ni kuenzi na kujifunza yale yote waliyoyaelekeza waasisi wa Taifa hilo kwa kuangalia “Mchango wa Mwalimu Nyerere katika mapambano dhidi ya rushwa.”

error: Content is protected !!