October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wapinzani wataisoma namba – Rais Magufuli

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Magufuli, amewaeleza wakazi wa Mwanza kwamba ‘wapinzani wataisoma namba.’ Ni baada ya kile alichoita ushindi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 7 Septemba 2019, katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa daraja la Kigongo – Busisi, jijini Mwanza.

Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, amepongeza viongozi na chama chake kwa ushindi mkubwa walioupata katika uchaguzi huo. Kwenye uchaguzi huo uliosuswa na vyama vya upinzani baada ya wasimamizi wake kuunajisi, uliipa ushindi CCM kwa zaidi ya silimia.

“Niwashukuru sana madiwani na wabunge wote kwa kuendelea kuchapa kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania, niwashukuru sana viongozi wa chama changu mnafanya kazi kubwa.

“Hongereni kwa ushindi mkubwa mlioupata hapa, watendelea kuisoma namba wapinzani,” ameeleza Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amewataka Watanzania wakati wanajiandaa kusherehekea maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, wadumishe amani na upendo.

“Wakati tunajiandaa kusherehekea miaka 58 ya uhuru,  tuendelee kudumisha amani na upendo ili maendeleo haya yaweze kufanikiwa kikamilifu. Palipo na amani kuna maendeleo, pasipo kuwa na amani hata kujenga kivuko hiki ingekuwa ni shida,” ameeleza Rais Magufuli.

Amesema, nchi ina maendeleo kutokana na umoja wa wananchi, pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi zake ipasavyo.

“Tuendelee kuitunza amani yetu, tusibaguane kwasababu ya dini, sura na hata kwa sababu ya hali zetu. Sisi wote ni Watanzania na tuendelee kujijenga Tanzania.

“Mawazo yetu sisi wote tuwe Tanzania moja. Mambo haya yanaenda kwasababu tuko pamoja, vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi yake,” amesema Rais Magufuli.

error: Content is protected !!