January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wapinzani wamng’ang’ania Pinda

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kijibu maswali bungeni

Spread the love

KAMBI ramsi ya upinzani bungeni imembana tena Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ikisema ameshindwa kabisa kutatua migogoro mingi ambayo inajitokeza kati ya wakulima na wafugaji. Anaandika Danny Tibason … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa bungeni na msemaji mkuu wa Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Mkiwa Kimanga, alipokuwa akiwasilisha maoni ya kambi kwa hotuba ya makadirio ya matumizi na mapato ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2015/16.

Amesema kuwa waziri mkuu ameshindwa kutatua migogoro mingi ambayo imekuwa ikijitokeza kati ya wakulima na wafugaji.

Mkiwa amesema migogoro mingi kati ya wakulima na wafugaji imekuwa ikishika kasi na kutolewa taarifa bungeni lakini kutokana na uchovu wa Serikali, hakuna hatua yoyote ambayo imetekeezwa kwa ajili ya kutatua migogoro hiyo.

“Waziri Mkuu ambaye ndiye kiongozi mkuu wa shughuli za serikali bungeni, alikuwepo wakati mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM), akisoma taarifa ya kuwepo kwa migogoro ya ardhi ambayo ilitolewa bungeni na serikali iliipokea.

“Lakini katika hotuba ya waziri mkuu hakueleza chochote kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge hasa ya kamati ya Ole Sendeka, iliyohusu kutoa suluhisho la migogoro ambayo inaendelea nchini kote.

“Mfano mzuri wa migogoro ambayo serikali imeshindwa kuitatua na waziri mkuu hajatoa tamko lolote la kiutekelezaji ni pamoja na Kiteto, Mvomero, Kilosa, Rufiji Mahenge, Morogoro Kusini na Kaskazini,” amesema Kimwanga.

Amesema kambi rasmi ya upinzani inaposema kuwa CCM imechoka ni kutokana na serikali iliyopo madarakani kushindwa kutatua matatizo ambayo yameishafanyiwa utafiti.

Mkiwa ameongeza kuwa, serikali imeshindwa kuwasaidia wafugaji na badala yake wamekuwa wakikejeliwa na serikali yao kwa kuwataka wapunguze mifugo badala ya kupatiwa njia mbadala.

Amesema kitendo cha kuwataka wafugaji wapunguze mifugo bila kuwapatia njia mbadala ni dalili za kuwadhalilisha na kutokutambua mchango wao katika pato la tafa.

“Kuwaambia wafugaji wapunguze mifugo yao bila kuwaambia wakulima wa kahawa, korosho na pamba nao wapunguze mazao ni dalili za ubaguzi kwa wafugaji,” amesema.

Kuhusu masoko, amesema kuwa Tanzana imekuwa ikishindwa kuwatafutia masoko ya uahakika wafugaji hao na badala yake imekuwa ikiruhusu ununuzi wa nyama ya ng’ombe pamoja na kuku kutoka nje ya nchi.

Alisema kuwa hata hivyo, serikali imeshindwa kutafuta uwezekano wa upatikanaji na utunzaji wa maziwa pamoja na ujenzi wa viwanda vya uhakika.

Akizungumzia suala la uvuvi, amesema kuwa serikali haijatilia mkazo katika sekta hiyo kutokana na kutoutambua umuhimu wa sekta hiyo kutokana na kutowawezesha wavuvi.

error: Content is protected !!