Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wapinzani waibana Serikali mapendekezo kikosi kazi
Habari za Siasa

Wapinzani waibana Serikali mapendekezo kikosi kazi

Spread the love

 

WAKATI viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wakiitaka Serikali itoe ratiba ya utekelezaji mapendekezo ya kuboresha mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, ameitaka ipeleke muswada wa sheria ya upatikanaji tume huru ya uchaguzi bungeni, jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).

Ado alitoa wito huo jana Jumatano, katika ziara yake ya ujenzi wa ACT-Wazalendo, mkoani Kigoma.

Katibu Mkuu huyo wa ACT-Wazalendo, alisema chama chake kinataka mapendekezo ya wadau kuhusu upatikanaji wa tume huru ya uchaguzi, yafanyiwe kazi mapema kabla ya chaguzi zijazo, Uchaguzi Mkuu wa 2025 na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2025.

“ACT Wazalendo tunataka mapendekezo ya Kikosi Kazi, hasa kuhusu Tume Huru, yatekelezwe mapema. Serikali ipeleke mapema Muswada wa Kuudwa Tume Huru itayosimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Uchaguzi Mkuu na Kura ya Maoni ya Katiba Mpya,” amesema Ado Shaibu.

Wito huo wa Ado umekuja ikiwa zimepita siku kadhaa tangu Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, waliitaka Serikali itangaze ratiba juu ya utekelezaji wa mapendekezo hayo, yaliyolenga kuboresha mfumo wa demokrasia ya vyama vingi.

Upatikanaji tume huru ya uchaguzi, katiba mpya na uondoaji zuio a mikutano ya hadhara.

Mapendekezo hayo yalikusanywa na Kikosi Kazi kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kilichokuwa kinaongozwa na Mwenyekiti wake, Prof. Rwekaza Mukandala.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!