May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wapinzani wa Simba kucheza na Bayern Munich

Al Ahly

Spread the love

 

WAPINZANI wa Simba kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Afrika, Al Ahly kutoka Misri wanatarajia kuvaana na FC Bayern Munich kutoka Ujerumani kwenye hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Dunia. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Al Ahly ambayo ipo kwenye kundi A, ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika sambamba na Simba kutoka Tanzania, AS Vita ya Congo DR na El Merreikh kutoka nchini Sudan.

Klabu hiyo inashiriki michuano hiyo ikiwa kama bingwa ndani ya bara la Afrika, ambapo mara baada ya michuano hiyo itarudi tena kuanza tena mbio za kutetea taji hilo dhidi ya El Merreikh ya Sudan na tarehe 23 Februari 2021 itaikabili Simba kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam

Bao pekee la Al Ahly kwenye mchezo wa jana dhidi ya Al Duhail ya Qatar, lilifungwa na El Shahati kwenye dakika ya 30.

Ushindi huo utawafanya mabingwa hao wa Afrika kwa msimu wa 2019/20, kukutana na mabingwa Ulaya klabu ya Bayern Munich kwenye mchezo wa nusu fainali utakaopigwa tarehe 8 Februari 2021.

error: Content is protected !!