February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wapinzani DRC kumtikisa Kabila

Jean-Pierre Bemba

Spread the love

HATUA ya Mahakama ya Juu nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kutangaza kuwa, mgombea wa chama kikuu cha upinzani-MCL- Jean-Pierre Bemba hana sifa ya nafasi ya urais, inapeleka taifa hilo kwenye maandamano. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Tayari chama kikuu cha upinzani MCL nchini humo kinajiandaa kufanya maandamano kupinga kauli hiyo pamoja na uchaguzi mkuu ujao. Bemba ameondolewa kwenye orodha ya wagombea urais wan chi hiyo kwa madai ya kukosekana ushahidi wa kutosha pia mahakama kukosa imani na upande wa ushahidi katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.

MCL kinaendelea na vikao vya ndani ambapo taarifa ya awali imeeleza kuwa, watatangaza tarehe ya maandamano hayo na kwamba, uamuzi wa mahakama ya juu ni wa hovyo.

Pamoja na hivyo MCL inaituhumu tume ya uchaguzi ya nchi hiyo pamoja na mahakama nchini kuwa vinaendesha shughuli zake kwa kuegemea upande wa chama tawala.

Swali ni kuwa, je chama cha MCL kitaunga mkono mgombea mwingine kutoka kambi ya upinzani ambaye ana fursa ya kugombea nafasi hiyo au watabadili mwelekeo na kushughulika na mchakato mzima? Haijafahamika.

Bemba kwa sasa yuko mjini Brussels, alirejea mjini Kinshasa Agosti, lakini kurejea kwake tena nchini humo kumeahirishwa.

error: Content is protected !!