September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wapiga dili CCM kuhenyeshwa

Ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dodoma

Spread the love

ROBERT Mwinje (39) na  Nyemo Malendaa(20), wote makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Dodoma wanatarajiwa kupandishwa kizimbani muda wowote kutoka sasa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mwinje aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini na Malendaa, mhudumu wa ofisi hiyo wanakabiliwa na makosa ya kula njama, kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo za uteuzi wa waombaji uongozi ndani ya chama hicho.

Sosthenes Kibwengo, Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Dodoma amesema Mwinje na Nyemo waligushi barua ya uteuzi wa waomba uongozi ndani ya chama hicho.

Pia walidai imetolewa na uongozi wa chama wilaya ya Dodoma, wakaikabidhi kwa mwanachama mmoja kwa hatua huku wakifahamu kwamba ni uongo.

Mwinje aliondolewa katika nafasi yake hiyo ya uenyekiti hivi karibuni na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika jijini Mwanza. Kikao hicho kiliongozwa na Dk.John Magufuli, Mwenyekiti wa chama Taifa.

error: Content is protected !!