Monday , 26 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Wapiga debe Dar jino kwa jino na Polisi
Habari Mchanganyiko

Wapiga debe Dar jino kwa jino na Polisi

Lucas Mkondya, Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
Spread the love

JESHI la Polisi Kanda maalum ya jijini Dar es Salaam limeahidi kupambana na wapiga debe katika vituo mbalimbali vya mabasi na kuwakamata, anaandika Irene Emmanuel.

Hayo yamesemwaka leo na Kamanda wa Polisi kanda hiyo, Lucas Mkondya na kewamba kazi ya kuwasaka wapiga debe imeanza katika vituo vya mabasi.

Akizungumza na MwanaHALISI online, Mkondya amesema kuna mbinu nyingi ambazo watazitumia kupambana na wapiga debe hadi kuhakikisha wameondoka wote.

Amesema hawezi kusema mbiunu watakazotumia katika kufanikisha kazi hiyo, lakini akaahidi kwamba haitakuwa na kikomo.

‘Tukiwatoa huku wakajidanganya kukimbilia mtaani watakutana na sisi tena, kwa hiyo wao wafanye kazi zilizo halali na siyo za uhalifu kwani tutapambana nao.,” Mkondya ameeleza.

Amesema tayari wameishaanza kazi katika baadhi ya vituo vya mabasi ikiwemo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Hii siyo mara ya kwanza jeshi la polisi kupiga marufuku uwepo wa wapiga debe katika vituo vya mabasi bila mafanikio.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RC Geita awafunda wahitimu wapya GGML

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito kwa...

Habari Mchanganyiko

Biteko asisitiza umuhimu wa EREA sekta ya nishati

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Tembo aongoza migongano binadamu, wanyamapori

Spread the loveIMEELEZWA kuwa asilimia 80 ya migongano baina ya binadamu na...

Habari Mchanganyiko

“Watanzania tembeleeni vivutio vya utalii”

Spread the loveSHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limewataka Watanzania kujitokeza kutembelea...

error: Content is protected !!