September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wapaza sauti kuomba msaada

Spread the love
FAMILIA zilizoathirika na mvua zilizoambatana na upepo mkali katika kata tatu za Manispaa ya Dodoma, zimeomba msaada wa vyakula na mapaa, anaandika Dany Tibason.
Wakizungumza wakati wa kupokea msaada wa vyakula jana kutoka Jumuiya ya Ahamadia, wakazi hao wamesema, mvua hizo zimeharibu vyakula walivyokuwa wamehifadhi kwenye nyumba zao.
“Hapa nilipo unga wote niliohifadhi ndani umejaa maji, sina chakula ninaomba mnisaidie,”amesema Maria Dulu, Mkazi wa Kata ya Mkonze.
Tahir Mohamood Chaudhary, kiongozi wa dhehebu hilo amesema, wameguswa na mahitaji ya familia hizo na kuchanga fedha hizo kwa ajili ya kuwasaidia.
“Sisi sio matajiri, tumeamua kutoa hiki kidogo hiki tulichonacho kuwasaidia wenzetu waliokumbwa na mafuriko,”amesema.
Francis Monga, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi ameshukuru taasisi hiyo kwa wepesi waliouonesha kuzisaidia kaya hizo 50.
“Natoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuwasaidia watu wenye matatizo kama walivyofanya ndugu zetu hawa,”amesema.
Theobath Maina, Diwani wa Kata ya Ntyuka amesema, baadhi waathirika wa mvua hizo wameshindwa kurudishia mapaa ya nyumba zao na kuwafanya kuendelea kuishi kwa wasamaria wema.
“Baadhi ya kaya hazijaweza kurudisha mapaa kama unavyoona nyumba hii,”amesema huku akionesha moja ya nyumba iliyoathiriwa na mvua hiyo.
error: Content is protected !!