December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wapangaji sugu TBA wape wa siku 14

Spread the love

WAPANGAJI wa nyumba za serikali, wamepewa siku 14 na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kulipa malimbikizo ya madeni yao kabla haijawaondoa kwa nguvu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Agizo hilo limetolewa leo tarehe 1 Julai 2019 na Said Mndeme, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miliki TBA wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Mndeme amesema wadaiwa hao sugu kama hawatalipa madeni yao baada ya siku hizo kuisha, TBA itawachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani.

Mndeme amesema TBA inadai baadhi ya wapangaji wake malimbikizo ya kodi kiasi cha Sh. 10 Bilioni.

Wakati huo huo, Mndeme amewataka watumishi wa umma waliohamishwa vituo vya kazi huku wakiwa wanadaiwa na TBA, kulipa madeni yao ndani ya muda uliotolewa.

error: Content is protected !!