August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Wapalestina wanapaswa kuishi kwa amani’

Spread the love

VYOMBO vya Umoja wa Mataifa (UN) vimetakiwa kuhakikisha kuwa, raia wa Palestina wanaishi kwa amani kama ilivyo raia katika nchi nyingine zenye amani, anaandika Regina Mkonde.

Kauli hiyo imetolewa jana na Shehe Hemed Jalala, Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia nchini wakati akiazimisha Siku ya Quds ambayo ni Siku ya Kumbukumbu kwa Walapalestina.

“Tunaomba vyombo vya Umoja wa Mataifa na wadau wote wa amani duniani kuhakikisha kuwa Wapalestina wanaishi kwa amani.

“Waishi kama Waislamu, Wakristo pamoja na dini nyingine wanavyoishi mfano ikiwa ni sisi hapa Tanzania,” amesema.

Jalala amesema kuwa, mauaji na mateso yanayowapata Wapalestina kwa miaka mingi sasa ni kutokana na dhuluma, unyonyaji, ukandamizaji wanaofanyiwa.

Kwa muda mrefu sasa ardhi ya Palestina imekuwa ikikaliwa kimabavu na Israel jambo ambalo limesababisha kuibuka vya vita vlivyodumu kwa muda mrefu sasa.

Dunia imekua ikiilalamikia Israel kwa kuendesha mashambulizi na kuua watu wengi wa Palestina ambapo nayo (Palestina) ikijibu mashambulizi hayo kwa udhaifu.

“Siku hii ya leo Waislamu wa Tanzania hususan Msikiti wa Kigogo Posti unakumbuka Siku ya Quds duniani kwa namna nyingine ni Siku ya Palestina duniani.

“Kwa nini tunaikumbuka siku hii? Unapoangalia historia ya Palestina pamoja na ardhi yake, matendo yanayotendeka ni ya dhuluma na ukatili,” amesema Shehe Jalala.

Amesema, hakuna shaka kwamba ardhi ya Palestina haiko chini ya Wapalestina.

“Ni kitu cha kawaida nyumba za Wapalestina kuvunjwa kila siku, iwe ya Muislamu na hata ya Mkristo sambamba na uvunjwaji wa nyumba za ibada, haijalishi kuwa ni Msikiti wala Kanisa,” amesema na kuongeza;

“Na si ajabu kwa mama mjazito wa kipalestina kujifungulia njiani kwa sababu ya vizuizi vya Wazayuni.”

Shehe Jalala amesema kuwa, haipiti siku pasipo wapalestina kufa na au nyumba zao kuvunjwa.

“Huu ni uvumilivu ambao haukubaliki na haustahili kunyamaziwa,” amesema.

error: Content is protected !!