July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waombwa kuchangia safari ya India

Moja ya misitu iliyopo Tanzania

Spread the love

WATANZANIA wameobwa kuchangia nauli na misaada mbalimbali kwa ajili ya safari ya kwenda nchini India, yenye lengo la kuelimisha dhana nzima ya utunzaji mazingira hasa misitu na kupunguza hewa ya ukaa inayochochea ongezeko la joto duniani. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Hatua hiyo inakuja baada ya kuwepo kwa vifo zaidi ya 2000 nchini humo kutokana na wimbi kubwa la upepo unaoambatana na joto kali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Askofu Charles Gadi wa huduma ya Good News for All Ministry, amesema mbali na kutoa elimu, lengo lingine la safari hiyo ni kutoa misaada kwa makundi ya yasiojiweza wakiwemo watoto, wazee na masikini ambao ndio waathrika wakubwa wa hali ya joto kali nchini India.

Gadi ambaye pia ni Mwenyekiti wa huduma hiyo, amesema “hivi karibuni imeripotiwa kuwa wimbi kubwa la upepo wa joto limeikumba nchi ya India na kuua zaidi ya watu 2000 na bado wengine wanaendelea kupoteza maisha yao. Cha kusikitisha, waliokufa wengi ni wazee, masikini na watoto ambao hawana uwezo wa kujikinga na joto amabalo linahitaji matumizi ya viyoyozi na maji baridi,”.

“Kwa sababu hiyo, tumesukumwa na Mungu kuandaa mkutano wa maombi huko India. Tutaambatana na wachungaji zaidi ya 10 na waandishi wa habari kadhaa ili kufanya maombi yatakayoambatana na kutoa misaada kwa waathirika wa upepo wa joto kali,” amesema Gadi.

Gadi ameeleza kuwa, Watanzania pia wanapaswa kujua hali ya joto la dunia sio nzuri hasa, kutokana na taarifa za mara kwa mara za kupungua kwa barafu ya mlima Kilimanjaro na kuyeyuka kwa mabonge ya barafu katika mabara ya barafu ya Actic na Antarctica.

Taarifa hizo za kisayansi zinaonesha kuwa ongezeko la joto linatokana na uharibifu wa mazingira na kuongezeka kwa hewa ya ukaa duniani.

Akizungumzia kuhusu suala lililoibuliwa hivi karibuni la ulevi uliokitihiri katika Wilaya ya Rombo, Gadi amesema “sisi tunatoa ushauri kuwa uwepo mjadala wa wazi juu ya tatizo hilo la ulevi badala ya kutumia nguvu nyingi kumkemea Mkuu wa Wilaya aliyejaribu kutumia nguvu zake kukomesha unywaji huo mbaya wa pombe,”.

“Inasemekana ndani ya wilaya hiyo kuna aina za pombe za kienyeji 50. Hazina viwango vya TBS. Baadhi yake zina kilevi zaidi ya asilimia 58 hali ambayo ni hatari kubwa kwa maini na fizo za wanywaji. Uwezekano wa kupunguza nguvu za kiume upo,” ameeleza Gadi. 

error: Content is protected !!