January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanne wahukumiwa kifo kwa kuua Albino

Baadhi ya viongozi wal;itoa tamko juu ya mauaji ya albino

Spread the love

HATIMAYE Mahakama imetenda haki kwa familia ya marehemu Zawadi Magindu (22)-mlemavu wa ngozi (Albino), aliyeuwa na kisha baadhi ya viongo vyake kunyofolewa mwaka 2008. Anaandika Mwandishi wetu…(endelea).

Sasa watu wanne; Masalu Kahindi (54), Ndahanya Lumola (42), Singu Siyantemi (49) na Nassor Said (47) ambaye ni mume wa marehemu Zawadi, wamehukumia kunyongwa hadi kufa baada ya mahakama kuwatia hatiani kutenda unyama huo.

Hukumu hiyo, imetolewa katika siku ambayo Rais Jakaya Kikwete anakutana na walemavu hao Ikulu jijini Dar es Salaam ili kujadiliana namna ya kukomesha mauaji hayo nchini.

Bila shaka hukumu hii iliyotolewa leo na Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza katika kesi Na.43/2009, itakuwa “faraja” na watu wenye ulemavu wa ngozi.

Akitoa hukumu hiyo, Jaji wa Mahakama hiyo iliyoketi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, Joaqueen Demello, amesema kuwa mahakama yake imejiridhisha kwa ushahidi uliolewa mahakamani hapo na kubaini kuwa watuhumiwa hao walihusika na mauaji ya Zawadi.

Kwa mujibu wa Jaji Demello, ushahidi wa mashahidi 12, akiwemo mama wa mzazi wa Zawadi- aitwaye Magdalena na mtoto wa marehemu aitwaye Semen, uliotolewa mahakamani hapo, umetosha kuwatia hatiani watuhumiwa.

Amesema kuwa ushahidi huo unathibitisha bila shaka kwamba watuhumiwa wote, walihusika kumuua kinyama Zawadi.

“Kwa kuwa tendo hilo ni la kinyama na hakuna mtu asiyejua kwamba watu wanaofanya vitendo hivi ni “wanyama”, nimewatia hatiani kunyongwa hadi kufa,’’amesema Jaji Demello.

 Jaji Demello alifafanua kuwa watuhumiwa hao wanayo haki ya kukata rufaa iwapo wanaona mahakama hiyo haikuwatendea haki.

Awali upande wa mashitaka, ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Hezron Mwashimba, ulidai kuwa; watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Machi 11, 2008, saa 1:00 usiku katika Kijiji cha Nyamalulu Kata ya Kaseme wilayani Geita.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kumuua Zawadi na kisha kumnyofoa baadhi ya viungo vyake vya miguu na mkono mmoja na hivyo mahakama iliombwa itoe adhabu kali ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

error: Content is protected !!