WANAWAKE wanaoishi katika jamii zenye uhifadhi na usimamizi shirikishi wa misitu wameonesha mabadiliko makubwa katika kusimamia na utumiaji wa rasilimali hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).
Hayo yamesemwa na Ofisa Muhahamsishaji wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Saimon Lugazo wakati wa warsha iliyohusisha asasi mbalimbali zinazojishughulisha na rasilimali misitu ambazo ni mwanachama wa Chama Cha Wafanyakazi za Misitu Tanzania (TFWG).
Lugazo amesema bado hakujakuwa na idadi ya sawa kati ya wanaume na wanawake, ila ni wazi kuwa wanawake wameamka hasa kwenye suala la umiliki wa ardhi, kufanya biashara za misitu na kushiriki katika vikundi vya hisa.
Kwa upande wake Mtafiti Emmanule Mroto amesema katika utafiti huo wamebaini ongezeko la wanawake kujishughulisha na ukataji mkaa na kuwaweza kufungua miradi mbalimbali na kushauri vijana nao wanahamasishwe vya kutosha kushiriki katika mradi.
Nao baadhi ya washiriki wa warsha hiyo akiwemo Marygoreth Lwekiza kutoka Shirika la Mpingo na Mandeleo (MCDI), Fadhila Kateta kutoka Jumuiko la Maliasili Tanzania na Isaya Sekibo kutoka Suredo wamesema kuwa miongoni mwa shughuli kubwa wanazozifanya na kuhakikisha wanawake wanashirikishwa vya kutosha katika shughuli za misitu.
Warsha hiyo ambayo imehusisha wanachama TFWG imewezeshwa na Mradi wa Kuhifadhi Misitu kupitia Biashara Endelevu ya Mazao ya Misitu (CoFoReST ) unaoendeshwa na TFCG na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswizi (SDC).
Leave a comment