September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wanawake ‘waula’ bima za magari

Spread the love

WANAUME wengi hupata ajali za barabarani kulinganisha na wanawake kutokana na uendeshaji usio salama ikiwamo mwendo kasi na kuendesha magari mabovu, anaandika Josephat Isango.

Patrick Lodamun Afisa masoko wa kampuni ya Bima R&R jijini Dar es Salaam ambapo amesema kutokana na hali hiyo kampuni yao imeleta bima maalumu kwa wanawake wenye kumiliki magari yenye gharama ya Sh. 10 milioni na kuendelea kama zawadi kwa wanawake.

Lodamun amesema bima hiyo inaitwa Diva Motor ambayo imeandaliwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya first Assurance itasawasaidia wanawake wanaopata ajali za barabarani kwa hali na mali ikiwa ni pamoja na kuwalipa asilimia 95 ya gharama za magari pale yanapoharibika ajalini.

Ameongeza kuwa kutokana na wanawake wengi kubeba watoto kwenye magari yao wameamua kulipa fidia kwa siti zinazoharibika (Car sit), huku wakisaidia gharama za malazi iwapo mteja atapata ajali na kushindwa kuendelea na safari.

“Endapo ajali itatokea sehemu yenye umbali na uendapo utaruhusiwa kulala hoteli yoyote iliyokaribu na eneo la tukio na kampuni itagharimu kulipia gharama zote atakazozitumia akiwa hapo kwa muda huo,” amesema.

Vile vile endapo gari litaharibika mmiliki wa gari atapewa gari la kutembelea kwa muda wa siku 7 huku matengenezo ya gari yakitumia siku 14 pekee.

Amesema lengo la kutoa ofa hiyo kwa wanawake wanaamini itawanufaisha kwa namna moja ama nyingine ikiwemo fedha za matengenezo yanayo gharamiwa na kampuni hiyo zitafanyia mambo mengine ya kimaendeleo.

error: Content is protected !!