Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Wanawake, watoto 60 waliotekwa waachiwa huru
Kimataifa

Wanawake, watoto 60 waliotekwa waachiwa huru

Spread the love

 

ZAIDI ya wanawake na watoto 60 waliotekwa nyara wiki iliopita na watu wanaoshukiwa kuwa ni wanajihadi, huko kaskazini mwa Burkina Faso wameachiliwa huru. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Vikosi vya usalama nchini humo viliendesha oparesheni ya uokoaji wa kundi hilo la watu na kuwapata wanawake 27 watoto na wasichana wapatao 39, jirani na jimbo la kati ya Kaskazini.

Mamlaka nchini humo ilisema mapema wiki hii kwamba wahanga hao walitekwa nyara wakiwa katika shughuli za utafutaji matunda pori na vyakula vingine.

Tukio la utekaji nyara wa idadi kubwa ya watu nchini humo haujawahi kushuhudiwa licha ya taifa hilo la Afrika Magharibi kukabiliwa na uasi uliokithiri wa itikadi kali uliofungamana na makundi ya dola la kiislam na Al-Qaeda ambao umeenea nchi jirani ya Mali tangu 2015.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini

Spread the love  KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Jumamosi...

Kimataifa

Polisi ahukumiwa kifo kwa kumuua wakili

Spread the love  MAHAKAMA kuu nchini Kenya imemhukumu kifo Ofisa wa Polisi,...

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

error: Content is protected !!