August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanawake wapewa somo la unyonyeshaji

Mama akinyonyesha mtoto

Spread the love

WANAWAKE wamehimizwa kunyonyesha watoto kwa kipindi kinachoshauriwa kitaalamu ili kuwaepusha na madhara ya utapiamlo na udumavu wa akili, anaadika Mwandishi Wetu.

Mratibu wa Jinsia na Lishe wa Shirika la Taha, Salome Stephen alisema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa Kamati za Lishe za Wilaya ya Babati Mjini na Babati Vijijini ili kufahamu changamoto wanazokabiliana nazo.

“Jamii inatakiwa kuwa makini zile siku 1000 tokea ujauzito umeingia kumlea vizuri mtoto ambazo ni sawa na ile miezi tisa ya ujauzito na miaka miwili baada ya kuzaliwa mtoto,’’ amesema

Mtaalamu huyo wa masuala ya lishe alisema iwapo wazazi wakikosa hasa wakina mama wakashindwa kuwanyonyesha watoto kwa kipindi cha miezi sita mfululizo na wakawapa vyakula vingine kama vile uji ndio watakuwa wamearibu mtoto au watoto kiakiri.

“Kama wazazi wakikosea kumpa mtoto vyakula vya kumjenga kiakiri ndani ya siku 1000 hakuna tena wakati wa kuweza kurekebisha na kuondoa makosa uliyoyafanya hivyo wanatakiwa kua makini kipindi hicho,’’ alisisitiza.

Aidha, aliwataka wanawake kuwanyonyesha watoto wao kikamirifu kutwa mara kumi ila isipungue ndipo wanaweza wakawaepusha na utapiamlo na kuwaandalia mazingira rafiki ya kuja kufanya vizuri watakapoanza masomo.

error: Content is protected !!