June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wanawake wamkabidhi changamoto sita Rais Samia

Spread the love

 

WANAWAKE wa Mkoa wa Dodoma, wamemkabidhi changamoto sita Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, wakimuomba azitatue ili kuleta ustawi wa kundi hilo nchini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Changamoto hizo zimetolewa leo Jumanne, tarehe 8 Juni 2021 na Joyce Kashozi, akisoma risala ya wanawake hao, katika mkutano wao na Rais Samia, uliofanyika jijini Dodoma.

Kashozi ametaja changamoto hizo ni, ukosefu wa maji safi na salama katika baadhi ya maeneo hasa ya vijijini, ukosefu wa fedha za kutosha za mikopo inayotolewa na halmashauri na upungufu wa watalaamu, vifaa tiba na miundombinu ya sekta ya afya.

Nyingine ni, upungufu wa walimu na miundombinu ya sekta ya elimu na ombwe la wanawake katika nafasi za uongozi na kwenye vyombo vya utoaji maamuzi.

Akisoma risala hiyo, Kashozi amesema changamoto hizo zinarudisha nyuma maendeleo ya wanawake, na kwamba zinapaswa kutafutiwa ufumbuzi.

“Changamoto hizi ikiwemo uwiano usiolingana kati ya wanawake na wanaume, katika nafasi mbalimbali za uongozi na ufanyaji maamuzi, mila na desturi potofu zinazokandamiza wanawake, zikitatuliwa zitaleta ustawi wa wanawake nchini,” amesema Kashozi.

error: Content is protected !!