October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanawake wafanyabiashara 35 wapatiwa tuzo za umahiri

Spread the love

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, amekabidhi jumla ya tuzo 35 za umahiri kwa wanawake wafanyabiashara zilizotolewa na Chama cha wanawake wafanyabiashara (TWCC). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Waziri Gwajima, amekabidhi tuzo hizo jana wakati wa hafla ya kumaliza siku ya wanawake iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Dk. Gwajima amesema wanawake wanaweza kufanya mambo makubwa kwenye jamii na amewataka wanaume kuwapa nafasi ya kwenda kufanya biashara.

Aidha amekipongeza chama cha wafanyabiashara wanawake (TWCC), kwa kuandaa tuzo hizo na amewataka mwakani waongeze idadi ya tuzo hizo hata zifikia 150 ili kuendelea kuwapa moyo wanawake kuendelea kufanya vizuri kwenye biashara.

“Hizi ni tuzo muhimu sana kwa wanawake na nawashukuru wafadhili wa tuzo hizi na nawapa changamoto TWCC, ongezeni idadi ya tuzo hizi hata zifikie 100 na hii itasaidia kuwapa moyo wanawake kwamba wanaweza kufanya mambo makubwa,” amesema

Amesema ni muhimu wanawake wakafanyabiashara na kuinua kipato cha familia badala ya kumwachia mzigo baba peke yake kwani hali hiyo inaweza kumsababishia msongo wa mawazo na kusababisha apate maradhi au kifo cha mapema.

Amesema kuna fursa nyingi za mikopo ya riba nafuu ambayo imekuwa ikitangazwa na serikali na taasisi nyingi za fedha hivyo ni wajibu wa wanawake kuzifuatilia na kuzichangamkia kila zinapotokea.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa TWCC, Mwajuma Hamza amesema kulikuwa na majaji watano kutoka taasisi mbalimbali ambao walichuja majina ya wafanyabiashara hao kutoka kwenye sekta 16 zilizokuwa zikishindaniwa.

Amesema tuzo hizo zilitolewa baada ya maonyesho ya wiki moja ya maonyesho ya wanawake wajasiriamali yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ).

Amesema baadhi ya vigezo walivyoangalia ni uendelevu wa biashara husika ili wasimpe mtu tuzo na biashara yake ikafa na waliangalia pia mikakati ya biashara husika.

Ameongeza, kigezo kingine ni biashara iwe imerasimishwa na iwe na nembo ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na umiliki wa biashara husika.

Mbali na GIZ wafadhili wengine ni Trade Mark East Africa, CRDB, NMB, NBC,

error: Content is protected !!