Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000
Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love

 

ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya Lunguya Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kilomita 15 kufuata huduma za Afya Lunguya baada ya mgodi uliopo katika eneo hilo kujenga Zahanati kijijini hapo. Anaripoti Paul Kayanda, Kahama … (endelea).

Hatua ya ujenzi wa kituo cha afya ni juhudi za kikundi cha wanawake wanaojishughulisha na shughuli za uchimbaji wa dhahabu katika Halmashauri ya Msalala ambacho kilipewa dhamana na serikali ya kusimamia maduhuli na tozo mbalimbali kwenye eneo lenye mfumuko wa madini ya dhahabu ‘rush’ katika kijiji hicho.

Wakizungumzia ujenzi wa zahanati hiyo ambayo imekamilika kwa asilimia 80 baadhi ya wanawake hao Semeni John ambaye pia ni mwenyekiti wa mgodi huo wamesema wanajivunia kujenga Zahanati kupitia fedha za wajibu wa kampuni kwa jamii (CSR).

Amesema fedha hizo kiasi cha Sh milioni 200 waliyokusanya imewezesha zahanati hiyo kujengwa hadi kufikia asilimia 80 ya ujenzi.

Naye Katibu wa mgodi huo, Hilda Jackson amesema wataendelea kuhamasisha wanawake kuingiza kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu badala ya kuwaachia wanaume peke yao.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kijiji cha Nyamishiga, Diwani wa Kata ya Lunguya, Benedicto Manwari amesema wananchi wamefurahishwa na kitendo cha mgodi kuangalia eneo muhimu la huduma ya wananchi wote.

“Changamoto ya wananchi kuhangaika kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta matibabu inaondoka, mpaka sasa wananchi wanapata huduma kwa tabu kwani wanalazimika kutembea umbali mrefu wa kilomita 15 kwenda Lunguya Katani.

“Nyakati za usiku ni shida, wajawazito wanaofikia muda wa kujifungua ikitokea amepatwa na uchungu usiku ni shida,” amesema Diwani huyo.

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala, Flora Sagasaga amesema uwepo wa zahanati hiyo itasaidia pia wachimbaji wadogo wanaofanya shughuli zao kwenye mgodi huo pindi wanapopata majeraha madogomadogo.

Aidha, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo mkoa wa Shinyanga, Hamza Tandiko ameiomba serikali kupitia tume ya madini iwarasimishe akinamama hao na kuwapatia leseni ya uchimbaji ili wakusanye vyema maduhuli ya serikali pamoja na kuendelea kunufaisha wakazi wa Kijiji na maeneo mengine.

Naye Afisa Madini Mkazi mkoa wa Kimadini Kahama, Mhandisi Jeremia Hango akijibu ombi la leseni kwa akina mama hao amesema atalifikisha kwa wahusika wa kitengo cha leseni makao makuu jijijini Dodoma.

Amesema wanawake hao iwapo watapata leseni watachimba kwa bidii na tija zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania yakabidhi rasmi msaada nchini Malawi

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Bashe: Tumeshagawa pikipiki 5,500 kati ya 7,000 kwa maafisa ugani

Spread the love  WAZIRI wa Kilimo, Hussen Bashe, amesema wizara hiyo tayari...

Habari Mchanganyiko

Spika Tulia awapa neno mawaziri utekelezaji mashamba ya pamoja

Spread the love  SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amewataka mawaziri kushirikiana...

Habari Mchanganyiko

Ukosefu wa maadili kwa wakunga, wauguzi bado changamoto

Spread the loveIMEELEZWA kuwa vitendo vya uvunjifu wa maadili kwa  wauguzi na...

error: Content is protected !!