January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanawake waaswa kupima afya ya uzazi

Spread the love

WANAWAKE wametakiwa kupima afya zao mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa mbalimbali yanayoshambulia mfumo wa uzazi na kusababisha ugumba na vifo. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Ushauri huo umetolewa na Mwakilishi wa Marie Stopes, Debora Mugagi katika maadhimisho ya Siku Kimataifa ya Vijana yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es salaam.

Mugagi amesema wanawake wanatakiwa kupima na kujua afya kwa sababu dalili za ugonjwa wa kansa ya kizazi hazijitokezi hadi athari za ugonjwa huo zinapokuwa kubwa na kushindwa kutibika.

Aidha amesema ugonjwa huo husababishwa na ngono na kupelekea kifo au kumsababishia mwanamke ugumba kutokana na kuondolewa kwa mfuko wa uzazi.

“Hatua za awali za ugonjwa huo zinatibika, hivyo wanawake wanatakiwa kupima afya zao mara kwa mara kwa sababu ugonjwa huo hauna dalili,” amesema Mugagi.

Miongoni mwa vijana waliojitokeza kujifunza masuala ya afya ya uzazi, Nicole Ephram amesema kuwa amenufaika kujua umuhimu wa kupima afya ya uzazi mara kwa mara kwani inasaidia kujikinga na kulinda kizazi.

 

error: Content is protected !!