August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Wanawake saidieni vita dhidi ya dawa za kulevya’

Regina Chonjo, Mkuu wa wilaya ya Morogoro

Spread the love

REGINA Chonjo, Mkuu wa wilaya ya Morogoro amewataka wanawake nchini kutoa ushirikiano katika kufichua wanaohusika na biashara ya dawa ya kulevya ili kurahisisha vita dhidi ya biashara hiyo inayoshamiri kwa kasi, anaandika Christina Haule.

Chonjo ameyasema hayo leo kwenye sherehe za siku ya wanawake duniani zilizofanyika kimkoa katika uwanja wa Jamhuri.

“Wanawake ni nguzo kuu ya familia, hakikisheni mnatoa ushirikiano wa kutosha katika vita ya dawa za kulevya ili kuwanusu watoto na Taifa kiujumla kwani nguvu kazi inapotea kutokana na vijana kujiingiza kwenye dawa ya kulevya.

“Kauli mbiu ya siku ya mwanamke duniani inayosema Tanzania ya viwanda mwanamke ni msingi wa mabadiliko kiuchumi na iwe chachu ya kumuwezesha mwanamke kiuchumi,” amesema.

Amesisitiza kuwa Serikali inafahamu umuhimu wa mwanamke ndiyo maana kuna dawati la jinsia ambalo limeweza kupunguza unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake kwa kiasi kikubwa na kwa sasa wanawake wengi wanaendelea kujishugulisha.

mjasiliamali Emmy Kiula ameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuanzisha Tawi la Benki ya wanawake mkoani Morogoro ili kuwawezesha kupata mikopo mikubwa tofauti na sasa ambapo wanapata mikopo midogo ya Sh. laki 6 hadi mil 5 kwa vikundi.

Naye Ernest Mkongo akizungumza Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa aliwaasa wanaume kuthamini mchango wa wanawake huku wakiwawezesha wanapokwama ili waweze kusonga mbele kiuchumi.

“Mafanikio ya mwanaume yapo nyuma ya msukumo na mtazamo mzuri wa kinamama, hivyo thamani yao inapaswa kuonekana ambapo ustawi wa mwanamke ni ustawi wa Taifa.

“Wanawake mjitambue kimajukumu na kufanya juhudi katika shughuli za kiuchumi ikiwemo kujiunga katika vikundi mbalimbali kupata elimu za mambo mbalimbali ikiwemo ujasiliamali,” amesema.

Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila tarehe 8 Mchi ikiwa ni kuenzi mchango wa mwanamke katika maendeleo ya jamii kiuchumi, kisiasa na kijamii.

error: Content is protected !!