Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Miradi ya ujenzi yawainua wanawake Ruvuma
Habari Mchanganyiko

Miradi ya ujenzi yawainua wanawake Ruvuma

Spread the love

KATIKA kuunga mkono kauli ya ‘Kazi iendelee’ iliyoasisiwa na Rais Samia Suluhu Hassan, wanawake kutoka mkoani Ruvuna wamejitosa katika kazi za ufundi ujenzi kuchangamkia fursa za miradi inayotekelezwa na Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yanajiri wakati wanawake wakizidi kuvunja dhana ya aina ya kazi zinazopaswa kufanywa na wanaume na wanawake hususani baada ya kuongezewa ari na Rais Samia aliyekabidhiwa jukumu la kuiongoza nchini.

Wakizungumza na Mwanahalisi Online wanawake hao wanaoshiriki ujenzi wa Kituo cha Afya Lilambo kilichopo katika Kata ya Lilambo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Mmoja wa wanawake hao, Tatu Mwamizi ambaye kazi yake kubwa ni kuchanganya mchanga na kubeba kokoto anaeleza kwamba ujenzi wa miradi hiyo ya Rais Samia imewawezesha wanawake hao kusomesha watoto wao na pia kujikimu na hali ya maisha.

“Nikipata hela naweza kumnunulia mwanangu daftari na chakula, ile akiba inayobakia ninamnunulia sare za shule na kama kuna kifaa kimeisha,”

Naye Halima Mohamed ameeleza kwamba hapo awali hali yake ya maisha ilikua ngumu tofauti na sasa alipoanza kufanya kazi ya ujenzi katika miradi hiyo iliyoanza hivi karibuni.

“Hali yangu kidogo ilikuwa ni ugumu wa maisha nilikua nayumba-yumba jinsi ya kumsomesha mwanangu lakini sasa hivi namshukuru Mungu… hapa ninavyofanya kazi inanisaidia mwanangu anaendelea vizuri na mimi mwenyewe naendelea vizuri napambana na kazi.

“Najisikia furaha Rais Samia anaendesha nchi yetu na sisi wanawake tusishangae ipo mwaka na sisi tutakuja kupambana na kazi ngumu tunafanya,” amesema Halima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB yafadhili ziara ya mafunzo machinga, bodaboda Dar nchini Rwanda

Spread the loveBENKI ya NMB imefadhili ziara ya siku nne ya mafunzo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

Habari Mchanganyiko

Wadau wataka kasi iongezeke marekebisho sheria za habari

Spread the love  WADAU wa tasnia ya habari wametakiwa kuongeza juhudi katika...

Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Spread the love  JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari...

error: Content is protected !!