July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanawake CUF wambana Shaka

KATIBU wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka

Spread the love

KATIBU wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka, emetakiwa kuwa makini katika matamko yake ili kujiepusha na uongo. Anaandika Mwandishi Wetu…(endelea).

Onyo hilo kali limetolewa na Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Wananchi (CUF) kupitia kwa Mkuu wa kitengo cha habari, Najma Khalfan Juma, wakati akizungumza na wandishi mjini Zanzibar.

Amesema kwamba “Shaka amenasibisha mikutano ya CUF kutumia nembo za Chama cha ASP, jambo ambalo ni ukiukwaji wa sheria namba 5 ya mwaka 1992 ya vyama vya siasa”.

Kwa mujibu wa Najma, jambo hilo si la kweli kwa kuwa “hakuna asiyeijua bendera ya Afro Shirazi Party”- kilichotokea kwenye mikutano ni vijana wengi kwa uzalendo wa nchi yao wameamua kuchukua vitambara vyenye rangi tatu.

“Shaka inafaa kuichambua  tafsiri ya sheria ilivyo badala ya kuichukulia sheria kijumla jumla,”amesema Najma.

Amefafanua kuwa kwa tafsiri ya sheria namba 5 ya usajili wa vyama vya siasa ya mwaka 1992, ili itambulike kuwa chama kinatumia bendera isiyo ya chama hicho ni lazima iwe imewekwa katika sehemu maalum zinazotumiwa na chama hicho kama matawi, majimbo au ofisi kubwa.

“Kama ni kwa mantiki hiyo basi CUF haikuvunja sheria kama inavyodaiwa na Shaka kwamba kwenye mkutano wetu, tulipeperusha bendera za Afro Shirazi Party,” amesema.

Najma anasema “imekuwa ni kawaida ya Shaka kutamka maneno yasiyo na kipimo wala mizani” ya kukisemea chama chake jambo ambalo linatia aibu kwa chama kikongwe kama hicho kuwa na viongozi wasiojielewa.

error: Content is protected !!