Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wanawake 252 wachuana Viti Maalum CCM Dar
Habari za Siasa

Wanawake 252 wachuana Viti Maalum CCM Dar

Spread the love

WANAWAKE 252 wamejitokeza katika mchuano wa kuwania nafasi tano za ubunge Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Leo tarehe 23 Julai 2020, wajumbe wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam, wanapiga kura za maoni kupendekeza majina matano ya wanawake wa CCM watakaowania ubunge Viti Maalum mkoani humo, katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.

Wajumbe hao wa UWT, wanafanya uchaguzi huo katika Ukumbi wa PTA-Sabasaba, wilayani Temeke.

Katika nafasi mbili za wabunge Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam, wanawake 166 wamejitokeza huku nafasi ya mbunge viti maalum kundi la walemavu wakijitokeza 18. Wanawake 24 wamejitosa kuwania nafasi moja ya kundi la wafanyakazi.

Huku nafasi ya moja ya Mbunge Viti Maalum kundi la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) wakijitokeza wanawake 20.

Akizungumza katika uchaguzi huo, Kate Kamba, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, amesema mchakato huo utakuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya wanawake waliojitokeza kugombea nafasi hizo.

Hata hivyo, Kate amesema mwitikio mkubwa wa wanawake kugombea nafasi hizo unaashiria uhuru wa kidemokrasia, huku akiwataka wajumbe wa mkutano huo kuchagua wawakilishi wenye sifa.

“Demokrasia imetanuka wagombea wnegi kuliko wapiga kura, tutakua na kazi ngumu lakini muhimu kuchagua wawakilishi wetu, safari hii wengi wameenda kwenye viti maalum lakini nataka niwapongeze wote waliokwenda kwenye majimbo,” amesema Kate.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!