WAFANYAKAZI wa Kiume katika kampuni ya Chloride Exide nchini Kenya, wametinga ofisini wakiwa wamevaa mavazi ya kike ikiwa ni mkakati wao wa kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya afya ya wanawake. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).
Kutokana na kalenda ya maradhi iliyotolewa na Shirika la Afya duniani (WHO) mwezi Oktoba kila mwaka ni mwezi maalum kwa ajili ya kuongeza uelewa kuhusu saratani ya matiti hasa kwa wanawake.
Wafanyakazi hao wamechukua uamuzi huo ikiwa sehemu ya maadhimisho ya siku ya saratani matiti duniani inayotarajiwa kufanyika mwezi huu.
Mtendaji Mkuu wa Chloride Exide aliongoza wafanyakazi wa kiume katika kampuni hiyo kuvaa mavazi ya kike, katika hafla ya wiki ya wateja iliyoafanyika kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.
Leave a comment