Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanaswa wakisafirisha dawa za kulevya
Habari Mchanganyiko

Wanaswa wakisafirisha dawa za kulevya

Pingu
Spread the love

WATU watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo la dawa ya kuleya aina ya bangi, anaandika Christina Haule.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Leonce Rwegasira tukio la kwanza lilitokea Septemba 26 saa 9 usiku katika eneo la Mikese mizani kata na tarafa ya Mikese wilayani Morogoro Vijijini.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Iddi Juma (42) dereva na mkazi wa Tabata Segerea jijini Dar es salaam na Aniset Ferdinand (30) mkazi wa Tabata Chang’ombe.

Kamanda Rwegasira amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na kupekuliwa na askari polisi waliokuwa doria na kukutwa na bangi viroba 6 inayokadiriwa kuwa na uzito wa kilo 80 wakiisafirisha kwenda Dar es salaam ikiwa kwenye gari lenye namba za usajili T438 ARN aina ya Toyota Corsa.

Amesema, watuhumiwa pamoja na gari wanashikiliwa na polisi kituo cha Mikese huku hatua za kuwafikisha mahakamani zikiendelea.

Katika tukio jingine Ally Daudi anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukamatwa na vichane 27 vya Mirungi akiwa amevihifadhi kwenye mfuko wa sandarusi wa rangi ya bluu.

Kamanda Rwegasira amesema, mtuhumiwa huyo alikamatwa na askari waliokuwa doria septemba 27 saa 10 jioni katika maeneo ya Vibandani Manispaa ya Morogoro na kwamba anatarajia kufikishwa mahamani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!